BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, June 15, 2010

'NAUMWA' NGOMA MPYA YA DNJ FAMILY

Msanii anayefanya vizuri katika anga ya muziki wa Bongo Flava kutokea Tanga ambaye kwa sasa maskani yake ni kule London nchini Uingereza Tizzle, akiwa na washkaji zake Damuz, Josh, D wanaotengeneza kundi la DnJ Familiy, wameachia ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la 'Naumwa'.

Akiongea na Blog hii Tizzle amesema kuwa, wameamua kuunganisha nguvu kwa pamoja na washkaji zake ili kila mmoja aweze kuonyesha kipaji chake na kufanya muziki wa bongo flava uzidi kujulikana kimataifa.

Tayari msanii huyo anatamba na ngoma yake ya 'Nameless' aliyomshirikisha Damuz, ambayo aliitengeneza pale Mzuka Entertanment Rec iliyopo East London chini ya producer Josh.

Pamoja na kuwa wanne katika kundi hilo lakini 'Naumwa' imefanywa na Tizzle, Damuz na Josh studio ikiwa hiyo hiyo Mzuka Rec. Kila la kheri kundi la DNJ Familiy.

Kabla ya kwenda nchini Uingereza Tizzle alikuwa anaishi pale Majani Mapana na baadae kuhamia Bara Bara ya 15.No comments:

Post a Comment