Thursday, June 30, 2011
Wednesday, June 29, 2011
NINAOMBA KURA ZENU ZA DHATI
Habari wadau wa vijimanbo vya tanga, natumai wote ni wazima wa afya tele, kama hivyo ndivo basi sote tumshukuru Mungu muweza wa yote. Nakuja mbele yenu siku ya leo kwa kusudi moja tu ambalo kwa hakika tutashirikiana kwa pamoja na naamini tutafanikiwa. Ni muda mrefu tangu tuwe pamoja tukipashana habari za Tanga na hata zile zinazojiri kutokea nyje yaTanga, ndugu zangu watanzania wenzangu na wale wote wanaotokea Tanga.
Kuna hii kitu inaitwa TANZANIAN BLOG AWARDS 2011, natumai mmeisikia. Lengo la kuandika waraka huu kwenu ni kuwaomba kura zenu ili Blog yenu ya vijimambo vya tanga iweze kuibuka kidedea katika mchakato huo ambapo imechaguliwa kwenye category kadhaa ambazo ni Best Informative - Entertainments, Best Entertainments, Best News, pamoja na Best Music.
Mambo yote haya ukiyatazama kwa kina yapo kwenye Blog hii na nimatumaini yangu mnayafurahia sana. Jinsi ya kupiga kura BONYEZA HAPA kisha tazama upande wa kulia utaona vipenge kadhaa pamoja na nilivyokutajia kisha piga kura yako palipoandikwa http://ankomo.blogspot.com ukishabonyeza kwenye kile kiduara unabonyeza palipoandikwa VOTE, na hapo utakuwa umeipigia kura Blog yako.
NASHUKURU SANA NA NIMATUMANI YANGU NITAPATA KURA ZENU. NAOMBENI SANA!!
Labels:
Mwandhishi: ANKO MO
Monday, June 27, 2011
Friday, June 24, 2011
GRAND MALT TANZANIA OPEN FILM FESTIVAL NI JUNI 27 JIJINI TANGA

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Wednesday, June 22, 2011
SIKILIZA 'MATHEMATICS' WIMBO MPYA WA ROMA!

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Tuesday, June 21, 2011
MISS TANGA 2011 NI ZUBEDA SEIF

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
KITABU CHA 'YALIYONIKUTA TANGA' KINAKUJA KAA TAYARI!!
……Kwa mujibu wa yule dereva teksi, tulikuwa tayari tumekwishafika katika eneo alilolitaja kuwa ni Four Ways, moja kati ya eneo maarufu linalokutanisha barabara nne mahali pamoja. Nilitulia tuli mule garini.
Pamoja na kwamba kulikuwa ni usiku lakini niliweza kuona baadhi ya majengo yaliyokuwa pembezoni mwa barabara kutokana na taa za gari zilizokuwa zikimulika wakati tunaikaribia kona ya kuingia upande wa kushoto, kitendo ambacho kingefanya tuiache ile barabara tuliyokuwa tunakuja nayo.
Jengo moja lenye ghorofa tatu lililojengwa vyema likiwa na ukurutu wa rangi ya manjano, lilikuwa upande wa barabara ya pili kulia kwetu. Kulikuwa kimya, taa zikiwa zimewashwa kila upande wa jengo, huku wadudu aina ya kumbikumbi wakiwa wanaruka ruka juu ya zile taa. Hapakuwa na mtu pale nje.
Mbele tena kwa upande wa ile barabara, kulikuwa na jengo jengine lenye ghorofa nne likiwa limepakwa rangi nyeupe. Chini ya jengo hili palikuwepo na fremu tano za maduka, sikufahamu yalikuwa maduka ya nini lakini palionekana penye biashara nzuri, yote yalikuwa yamefungwa wakati ule.
Watu watatu waliokuwepo nje ya lile jengo, niliwahurumia sana kutokana na ubaridi mkali ulioambatana na upepo uliokuwa unavuma. Wawili kati yao walikuwa wamejibanza kwenye moja ya viambaza vilivyoko pale. Walijifunika makoti huku wamelalia maboksi.
Mwengine ambaye niliweza kumuona vizuri alikuwa amekaa kwenye kiti, amevalia gwanda za rangi ya buluu huku ameshikilia rungu kwa mkono wake wa kulia. Ni mwanamke!!! Tena bila shaka alikuwa ni mlinzi.................................
KAA TAYARI, KINAKUJA HIVI KARIBUNI!!
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Tuesday, June 14, 2011
INATIA MOYO- ASANTE FRESH JUMBE KUTOKA TOKYO!

"Mkuu, Saluti. Kazi unayofanya ya kutangaza mkoa wetu, unastahili nishani. Tupo pamoja."
Fresh Jumbe- Tokyo.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Monday, June 13, 2011
MSIKILIZE ROMA NA UJIO WAKE MPYA!

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Thursday, June 9, 2011
KWA WANANCHI WA JIMBO LA BUMBULI- WASILIANA NA MBUNGE WAKO NDUGU JANUARY MAKAMBA

Mfumo huo utaanza kutumika tarehe 10 Februari 2011, baada ya kipindi cha elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo kuu kukamilika. Kwa kifupi, wananchi wanapaswa kutuma kero, maoni na ushauri kwa Mbunge ambaye kila siku, yeye na wasaidizi wake, watakuwa wanasoma meseji hizi na kuwajibu au kuwatafutia majibu.
Kama kuna taarifa za haraka ambazo inabidi Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri, au Mkuu wa Polisi wa Wilaya au Bwana Afya inabidi azijue, basi Mbunge atasaidia kuzifikisha kwa haraka zaidi.
Huduma hii haiondoi haja ya Mbunge kuendelea kutembelea Jimbo na kuonana na watu wake. Ni kwamba, simu au SMS, kama njia rahisi ya mawasiliano, hakuna haja ya kuacha kuitumia wakati wananchi wenyewe wanaitumia sana.
Inawezekana ikaonekana ni gharama kubwa kwa Mbunge lakini hata haiko hivyo, ni suala ya mazungumzo kati ya Mbunge na mitandao ya simu ili gharama iwe at cost na Mbunge bado anaweza kugharamia hili kwa nusu ya posho yake (wapo Wabunge ambao wamejitolea nusu mshahara kwa jambo moja au jingine - kwa Mbunge wa Bumbuli hili ni muhimu).
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Wednesday, June 8, 2011
Tuesday, June 7, 2011
BEKA KUTOKA THT NAE KUISINDIKIZA MISS TANGA 2011 JUMAMOSI

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
WAZIRI MKUU AKITETA JAMBO NA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOANI TANGA MJINI DODOMA

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Monday, June 6, 2011
LINAH KUISINDIKIZA MISS TANGA 2011 JUMAMOSI


'SIO YA KUKOSA'
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Thursday, June 2, 2011
HAWA NDIO WATAKAOIWAKILISHA TANGA KWENYE SERENGETI FIESTA FILAMU!
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Wednesday, June 1, 2011
'SISI TUTAIJENGA TANGA' GROUP MPYA KUTOKA TANGA!

Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Subscribe to:
Posts (Atom)