MBUNGE wa jimbo la Handeni,Abdallah Kigoda ameahidi kutoa ushirikiano kwa warembo baada ya kuibuka washindi katika kitongoji cha Handeni kwenda kambi ya miss Tanga. Dr.Kigoda alitoa ahadi hiyo juzi wakati wa sherehe za mapokezi ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM.
Alisema kuwa atatoa msaada kwa warembo hao ili kuwawezesha kufanya vizuri katika hatua ya kuwania kinyang'anyiro cha kumpata mrimbwende atakaye wakilisha Tanga kwa urembo.
Mjumbe huyo aliahidi kutoa fedha mara baada ya warembo hao walioshika namba ya kwanza hadi ya tatu kuimba na kukiomba chama cha Mapinduzi kuwapa sapoti katika kambi ya Miss Tanga
Alisema kuwa anatambua uwepo wa warembo hao na kwamba kushiriki mashindano hayo si tu ni moja ya ajira kwao bali pia wanaitangaza wilaya,mkoa na Taifa kwa Ujumla,
"Ni wajibu wangu na jamii kutoa msaada wa kila hali kwa warembo hawa ili waweze kufanya vizuri na kufikia malengo yao ya urembo"alisema Dr.Kigoda.
Pia alitumia nafasi hiyo kwa kuitaka jamii kuondoa mawazo potofu kuwa urembo ni uhuni badala yake waone ni moja ya michezo hapa nchini na kwamba ni ajira.
Alibainisha kuwa urembo ni ujumbe tosha wa kuitangaza wilaya na utalii wetu kupitia mashindano hayo hivyo ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunatoa ushirikiano wa kutosha kwa warembo hao.
Nae mgeni rasmi diwani wa kata ya Chanika,Mhe.Mwinshashi Uledi aliwataka warembo hao kuhakikisha wanafanya vizuri na kuzingatia nidhamu katika hatua hiyo ya miss Tanga.
Alisema hatua ambayo wameimaliza ni ndogo kwani wakifanya vibaya katika kambi ya miss Tanga ni sawa na kuitia doa wilaya ya Handeni na kwamba ameahidi kutoa ushirikiano kwa warembo hao pale watakapo kwama.
Warembo hao ni Mwajabu Juma (20) ambaye amepata redio aina ya sabufa yenye thamani ya laki mbili,Habiba Rashid (19) amezawadiwa godoro kwa kushika nafasi ya pili huku Amina Bakari (19)akipata dina seti mshindi wa tatu
Kambi hiyo inatarajiwa kuanza May 22 mwaka huu ,kwa ajili ya mashindano ya kuwatafura warembo watakaowakilisha mkoa wa Tanga katika mashindano ya Miss Tanzania yatakayofanyika hapo baadae.
Na Sophia Wakati, Handeni
No comments:
Post a Comment