BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, May 23, 2011

WAREMBO MISS TANGA 2011 WAINGIA KAMBINI!

Warembo wa Miss Tanga 2011 wameingia kambi rasmi siku ya jana katika hoteli ya Raskazoni kwa ajili ya kujiweka sawa na shindano hilo linalotarajiwa kufanyika June 11 katika hoteli ya Mkonge jijini hapa. Kampuni inayoratibu mashindano hayo New Face Entertainment imesema kuwa, warembo hao watapiga kambi hapo kwa muda wa siku 20 ili kujipanga vema.

Warembo wa Miss Tanga punde waliposhuka kutoka kwenye gari lililowaleta kunako Raskazoni Hoteli.

Warembo wa Miss tanga 2011

Kampuni ya Sofia Production ilikuwepo kuhakikisha kumbukumbu inatunzwa. hapa kijana Juma akiwa kazini.

Anaitwa Mamy.....alikuwa akiwahoji watu mbali mbali waliofika Raskazoni Hoteli...

Anaitwa Maximilan Luhanga, ndie mratibu wa Miss Tanga 2011 kupitia kampuni yake ya New face Entertainment.

Hapa akifanya mahojiano na mmoja wa waandishi wa habari kutoka Tanga Televisheni.

Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Bingwa, anaitwa Oscar Assenga nae alikuwepo.

No comments:

Post a Comment