BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, May 4, 2011

KWA MARA YA KWANZA MKOANI TANGA! MISS KOROGWE HIYOOOO

Waandaji wa kitongoji cha Miss Korogwe 2011 wakiwa katika pozi! Kupitia kampuni yao ya Shalola Suply ndio inaileta Miss Korogwe kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya urembo mkoani Tanga. Mchakato wa kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 umepamba moto huku kila kitongoji kikionyesha nia ya kutwaa taji hilo kubwa. Tayari kitongoji cha Tanga City Central kimeshatoa warembo wake pamoja na kitongoji cha Miss Handeni. Miss College ni tarehe 13 ya mwezi huu siku ya ijumaa na Miss Lushoto ni tarehe 21 ya mwezi huu siku ya jumamosi.

Msanii maarufu wa komedi nchini Masele akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa kitongoji kipya cha Miss Korogwe walipokutwa na kamera ya anko mo Blogspot.

Miongoni mwa warembo hao wa Miss Korogwe, watatu ndio watapata nafasi ya kuingia kambi ya Miss Tanga 2011 ambapo kilele chake ni June 11 siku ya jumamosi pale Mkonge Hotel, imeandaliwa na New Face Entertainment.

No comments:

Post a Comment