BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, April 30, 2009

NANI MKALI KWA INJILI NA UREMBO.?


Christine Shusho

Rose Muhando

Sema nani mkali kwa urembo na kuimba nyimbo za injili, tuma kura yako kwenye namba 071900010 au E-mail jmihiko@yahoo.com

MABOMU YA MBAGALA BADO KITENDAWILI



Eti wanaomba samahani!! Je watarudishaje roho za watu zilizopotea kwa mabomu kule Mbagala..? Inauma sana mjomba- Iliobaki sasa hizi kambi ni bora tufugie kuku, tupate mayai na nyama labda ndilo tutaloliweza!! Vibaka, vibaka wameingia kwenye nyumba za wahanga nna kuiba vitu vyao.....Aah wangefanya nini ikiwa hawajui kesho yao.? Natania tu Mjomba, ila nikipata nauli nitakuja kutoa pole na rambi rambi.


Wananchi wa mbagala kizuiani wakishangaa mabaki ya bomu lililoruka kilometa karibu nne, na kutua uraiani hapo.mpaka sasa ilitangazwa kuwa watu watatu walifariki huku wakiacha watu zaidi ya 70 wakiwa majeruhi.


Baadhi ya watu wakitoka kwenye maofisi yao baada ya waziri kutangaza hali ya hatari na kuamuru watu wote washuke kutoka magorofani.

Tuesday, April 28, 2009

FEROOZ KULETA SOKONI SAUTI NA VYOMBO MAY 4


Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Ferooz Mrisho anatarajia kuingiza albamu yake mpya sokoni iitwayo sauti na vyombo may 4,Albamu hiyo iliyozinduliwa kwa kishindo ndani ya ukumbi wa diamond jubilee ina jumla ya nyimbo kumi

Ferooz ameiambia Jiachie leo kuwa albamu hiyo itasambazwa na kampuni ya usambazaji hapa jijini ya GMC,na kuwa albamu hiyo itapatikana kila sehemu ikiwemo na mikoani,hivyo wapenzi wa muziki wa kizazi kipya wajitokeze kwa wingi kuinunua albamu hiyo yenye kila aina ya ladha.
Albamu hiyo imerekodiwa na prodyuza P-Funk a.k.a Majani ndani ya Bongo Records,aidha amezitaja nyimbo zilizomo ndani ya albam hiyo kuwa ni sauti na vyombo, Kwa Kupaa, Mr.Policeman ambayo inatamba kwa sasa kwenye vituo vingi vya redio, Receiption na nyinginezo.

Katika albamu hiyo amewashirikisha wasanii kibao akiwemo Matonya, Maunda Zorro, Durry Sykes pamoja na Chid Benz ili kuifanya iwe bomba na yenye ladha mchanhanyiko.

ABDUL AIBUKA KIDEDEA MAISHA PLUS!!

Mshiriki wa Maisha Plus Abdul, akikikabidhiwa pesa halali za Kitanzania shilinngi Million Kumi Taslimu kutoka kwa mdau aliyepewa jukumu la kutoa zawadi hiyo kunako usiku wa kuamkia jana wakati shindano hilo lilipofika tamati.

Katika siku hiyo ya mwisho washiriki kumi waliobakia walianza kutolewa kwa uchache wa kura walizokuwa wakipigiwa na watazamaji wa kituo cha televisheni cha TBC1. Washiriki walioingia kumi bora ni Boniface, Maulid, Upendo, Steve, Teddy, Charles, Moshy, Hamis (Kingunge), Modesta na Abdul. Baadaye wakatolewa Modesta aliyepata kura 620, Boniface (1,260) na Teddy (2,666). Wakafuata Kingunge (3,006), Moshi (3,828), Maulid (4,251) na Steve (5,700).


Ndipo wakabakia Upendo, Charles na Abdul. Akatolewa Upendo. Kazi ikabaki sasa kwa Abdul na Charles, marafiki wawili wakubwa katika kijiji. Na kama wengi walivyotabiri, Abdul aliondoka na Milioni 10 kwa kumbwaga Charles na wanakijiji wengine kwa kuwa na kura nyingi zaidi.


Washiriki hao walioingia kumi bora leo hii wanatembelea mbuga za wanyama Mikumi kwa ahadi waliyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwanguna, alipotembelea kijiji cha Maisha Plus wiki iliyopita.






Friday, April 24, 2009

BONGO STAR SEARCH DAR NI JUMAMOSI NA JUMAPILI.

Mkurugenzi wa Benchmark waandaaji wa Bongo Star Seach Ritah Paulsen (Pichani) akizungumza na wanahabari katika mako makuu ya Vodacom jengo la PPF Tower wakati alipoongea na wanahabari kuelezea juu ya shindano la BSS linalotarajiwa kufanyika jumamosi na jumapili mkoani Dar es alaam kulia ni Nector Foya meneja mawasiliano Vodacom.
Shindano la kutafuta wawakilishi wa mkoa wa Dar es alaam katika shindano la BSS 2009 litafanyika kuanzia jumamosi mpaka jumapili wiki hii katika ukumbi wa New World Cinema ambapo zaidi ya washiriki wapatao 2000 wanatarajia kujitokeza ambapo mshindi wa mwaka huu anatarajiwa kuondoka na zaidi ya milioni 15 ambazo mshindi wa mwaka jana alijishindia.
Kampuni ya simu za mkononi Vodacom ni wadhamini wa shindano hilo linaloratibiwa na kampuni ya Benchmark Production ambapo zaidi ya vijana 8000 wameshiriki katika mchujo huo mikoani kote ambako shindano hilo limefanyika na vijana 35 wameingia raundi ya pili ya shindano hilo vijana walishinda mikoani na mikoa yao ni kama ifuatavyo
.....Dodoma ni: Mwapwani Yahaya, Waziri Salum, Kamwitani Malili, Sarafina Mshindo na Joma Malick.
Mwanza ni Beatrice Wiliam, Haji Ramadhani, Monica Amon na Paschal Casian Tabora ni: Leah Julius, Rajabu Miraji na Kayombe Mrisho
Mtwara ni: Jamilah Yusuf, Josephat Obedi, Nicolaus Samuel na Ally Mtambo Mbeya ni: Ndigwabo Ahazi, Anitha Jackson, Issa Ahmed na Mosses Mwaifele
Arusha ni: Brandy Francis Amani Lisu, Sarah Mbwambo na Frola Ezekiel
Tanga ni: Jumanne Charles, Njele Juma, Jackson George na Marck Kauli
Kigoma ni: Peter J Msechu na Kauke Adam na mwisho ni Zanzibar ambako wamepatikana Mohamed Omary, Yusuph Mina, Aboubakar Pishak na Kelvin Stephen wasindi hawa wataungana wa watakaopatikana kutoka mkoa wa Dar es alaam na kuingia mzunguko wa pili wa mchujo huo.

Monday, April 20, 2009

MAISHA PLUS MAANA YAKE NINI..?


Waswahili wanasema Njaa kipimo cha akili, Kila kukicha watu wanazidi kubuni namna ya kukabiriana na maisha ya kila siku, na hii imekuwa changamoto kwani maisha ya kutegemea kuajiriwa kwa sasa hakuna na kila mmoja anatakiwa kuwaza jinsi gani atajiajiri. Changamoto hii ndio matunda ya vitu kama Maisha Plus.



Maisha Plus ni nini?Ni shindano la uhalisia ( Reality Show) ambayo halijawahi kufanyika barani Afrika, ni shindalo linalo ‘reflect’maisha halisi ya Mtanzania hasa vijana. Shindano hili lilianza kuonyeshwa kupitia kituo cha TBC1 March 1,2009, Mchakato wa kuwatafuta washiriki 18 ulianza Novemba mwaka 2008 katika kanda nane za Tanzania bara na Visiwani.



Lengo la Maisha Plus ni nini?Kuwawezesha vijana kujitambuaKuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali kupitia semina na mafunzo mbalimbali wanayopewa.Kuendeleza vipaji vyaoKuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki.Kubadilishana utamaduniKuburudisha watazamaji. Malengo ya badae ya Maisha PlusMwezi wa saba season II ya shindano hili itaanza na safari hii usaili utafanyika katika mikoa yote ya Tanzania.



Season III ya shindano hili itajumuisha nchi zote za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi n.k. Waandaaji wa shindano hili ni kampuni ya dmb Inc inayomilikiwa na Masoud Kipanya, Fransis Bonda na David Sevuri. Kipindi hutengenezwa na kampuni ya True Vision Production.



Regards

Julieth Kulangwa Media

Media Coordinator
0717 551355

KILIMANJARO IPO JUU - USIPIME!!

Wanamuziki Justin Timberlake,MC Lupe Fiasco na Kenna(huyu ana asili ya Ethiopia) kutoka nchini Marekani,wanatarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro baadaye mwaka huu katika kile kinachoelezewa kuwa kampeni ya kuelimisha na kuhamasisha masuala ya mazingira na upatikanaji wa maji safi duniani.

Huu ni wakati mwingine mzuri wa kutangaza utalii wa Tanzania.Kama ulivyo wewe,mimi pia nangoja kuona jinsi ambavyo Wizara ya Utalii,Bodi ya Utalii na Mamlaka za Hifadhi zitakavyochangamkia nafasi hii katika kuitangaza Bongoland.



Itakuwa mzuka kumuona mtu mzika Timberlake akikwea Mlima


Thursday, April 9, 2009

MMOJA WA AKINA DADA WANAOVUTIA KIMAPENZI TANZANIA- IRENE UWOYA


Irene Uwoya ambaye anashikilia taji la Miss Tanzania 4th Runner up 2006-07. Hivi sasa anajishugulisha na maswala ya filamu nchini Tanzania, vile vile ni mdau mkubwa wa mikao ya kimahaba. Kama utakuwa ni mtazamaji mzuri wa filamu za kitanzania, basi utakuwa unamfahamu vyema mwanadada huyu.


Mfano mtazame kwenye filamu inayoitwa Diversion Of Love jinsi ambavyo amevaa husika na namna alivyokuwa akijituma kuhakikisha hapwai sehemu yake. Huyu nye Irene Uwoya, mmoja wa akina dada wanaovutia kimapenzi nchini Tanzania.

JE TUTAFIKA KWELI KWA MTINDO HUU DADA YETU IRENE..?

Wednesday, April 8, 2009

HUYU NDIE MKALI WA HIP HOP TANZANIA

Jina lake ni Albert Mangwea. Kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya ukimuita Ngwea watakuelewa zaidi. Hivi majuzi alijishindia tuzo ya Kili Music Award kama Best Hip Hop Artist in Tanzania akiwashinda wakali wengine kama Fid Q, Chid Benz, Mwana FA na Witness.

Ngwea mwenyewe hakuwepo ukumbini wakati wa kutolewa kwa tuzo hizo na badala yake tuzo yake ilipokelewa na Meneja wake Tippo Athuman ambaye pia ndio mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions. Yawezekana Ngwea hakutokea kutokana na kubanwa na masomo pale Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambako amekwenda kujifunza mengi katika sanaa.

Sasa wengi mmeshamsikia Ngwea. Ametoka mbali mpaka kufikia hapo alipo! Lakini wengine wamejiuliza,kwanini kashinda? Kwa wale mlionitumia swali hilo jibu langu ni fupi;sijui.Lakini naweza kuhisi.Mwaka huu zipo nyimbo kadhaa za Ngwea ambazo zimetamba na kujikita vizuri katika vichwa vya watu.Miongoni mwa nyimbo hizo ni ule wa Nipe Deal ambao ulitengenezwa katika style kutoka “Bondeni”. Kama hujausikia basi leo tunakupa nafasi hiyo.





Monday, April 6, 2009

WAJUE WASHINDI WA TUZO ZA KILI AWARDS 2009

Chid Benz a.k.a King Kong pembeni na msanii kutoka nchini Marekani Chingy, alipomkabidhi msanii huyo tuzo ya wimbo boea wa Hip Hop ( Dar Stand Up ).


Makamua, Joslin pamoja na Q Jay wakifurahia kwa pamoja tuzo yao baada ya wimbo wao wa Natamani kuwa wimbo bora wa RnB


WASHINDI WENGINE NI PAMOJA NA.....


Mwimbaji Bora wa Kike- Keisha(pichani)
Mwimbaji Bora wa Kiume- Mb Dogg
Albamu Bora ya Taarab- VIP( Jahazi Modern Taarab)
Wimbo Bora wa Taarab- VIP(Jahazi Modern Taarab)
Wimbo Bora wa Mwaka- Anita (Matonya ft Lady JayDee)
Wimbo Bora wa Kiswahili- Heshima kwa Mwanamke (FM Academia)
Albamu Bora ya Kiswahili- Pekecha Pekecha(Akudo Impact)
Wimbo Bora wa R& B- Natamani (Q Jay ft Makamua & Joslin)
Albamu Bora ya Muziki Asilia- Dela Dela( Che Mundugwao)
Wimbo Bora wa Hip Hop- Ngoma Itambae(Chid Benz)
Wimbo Bora wa Reggae- Ripoti (Tunda Man)
Msanii Bora wa Rap- Mangwea
Wimbo Bora wa Afrika Mashariki- Salary(Nameless from Kenya)
Mtunzi Bora wa Muziki- Karama Legesu
Mtayarishaji Bora wa Muziki- Hammie B
Mwandikaji Bora wa Muziki- Prof.Jay
Wimbo Bora wa Zouk- Nalivua Pendo(Mwasiti)
Mtayarishaji Bora wa Video- Kallaghe Production
Wimbo Bora wa Collaboration- Anita (Matonya ft Lady Jaydee)
Wimbo Bora wa Asilia- Kazi ya Dukani(Dogo Mfaume)






Sunday, April 5, 2009

UNTOUCHABLE DJ'S- KITOVU CHA BURUDANI TANZANIA

Mshkaji anaitwa William J Lisingu, ni muanzilishi wa Untouchable Dj's ambayo kwa hivi karibuni imekuwa ikija juu sana kwenye anga za burudani ukizingatia ubunifu aliokuwa nao jamaa pamoja na ujuzi.

Untouchable kwa ujumla ilianzia jijini Tanga, takribani miaka miwili iliyopita wakati William akiwa na redio Mwambao fm. Ni ngumu kuelezea wazo la ujio wake wa Untouchable alikolipata, lakini kwa undani zaidi utagundua juu ya hisia kali za muziki ambazo jamaa anazo.


Wakati anapiga story na Blog hii, Will kamwe huwezi kumdhania kwamba anaweza kufanya mambo makubwa kama ambavyo tayari ameyafanya hadi sasa kupitia Untouchable.

Tayari Untouchable umemuwezesha kuwa na mradi wa fulana ambazo unawakilisha nembo ( LOGO ) za Untouchable. Awali wakati naziona fulana zake kwa mmoja wa watangazai mahiri wa Mwambao fm Bra-A, nilivutiwa sana.

Nikaona kuna haja ya kuwaletea kitu kizuri wadau wangu wote ambao wanashiriki kwa pamoja kuhakikisha Blog hii inapiga hatua. Kiukweli, ukizungumzia Dj's ambao wanafanya vizuri jijini Tanga na hata Tanzania kwa ujumla- basi hutasita kutaja Untouchable Dj's ambao kiongozi wake ni William J Lusingu. Kama ulipata bahati ya kutazama video ya wimbo wa Angie ambao alimshirikisha Chid Benz, ngoma inaitwa WEWE- Utakubali kwa ninachosema hapa
.
Big sana kaka and keep it up!!!!




Friday, April 3, 2009

CHINGY KUKAMUA 'LIVE' TANZANIA



Msanii nyota wa Marekani, Chingy atapanda jukwaani katika
viwanja vya Leaders Kinondoni Machi 5 mwaka huu katika
tamasha la la Tuzo za muziki nchini za Kili Music Award
2009.


Msemaji wa onyesho hilo Hemed Kavi (HK) aliiambia blog hii
kuwa, wameamua kumleta msanii Howard Bailey Jr maarufu kama
Chingy ili kuleta ladha kwa wadau wa tuzo hizo nchini.
Tuzo za Kili Music Awards hutolewa kila mwaka nchini,
zinatolewa tena mwaka huu ambapo halfa hiyo inatarajiwa
kuhudhuliwa pia na wasanii wengi kutokea nchini Tanzania.

Mbali na Chingy lakini pia wasanii wa kundi zima la Blue 3
kutokea nchini Uganda linatarajiwa kutumbuzia siku hiyo
halikadhalika mzee wa Salary, Nameless kutokea nchini Kenya
nae atakuwepo.

Thursday, April 2, 2009

NAJUUUUUUTA KUKUFAHAMU!!!!


Joti akiwa mzigoni na kundi zima la Ze Comedy

'NAPENDA NINI' YA JAFARAI


Enzi zile alipoanza kutambulika rasmi ilitokana na wimbo wake uliokwenda kwa jina “Nipo Bize”.Si unakumbuka jinsi alivyokuwa akimwambia kimwana wake kwamba asimtafute kwa sababu yuko bize?



Basi yawezekana ni kweli kwamba mshkaji huwa yuko bize kwani Jafarai ameshakamilisha albamu yake mpya itakayokwenda kwa jina Wali Nazi. Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 9 ambazo zote zimerekodiwa katika studio za Fish Club za jijini Dar.Katika albamu hiyo Jafarai amewashirikisha wasanii wengine kama vile mwanadada Naazizi kutoka Kenya,Lamar ambaye pia ni producer wa albamu hiyo na pia Wateule.



Mojawapo ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni wimbo ambao unatamba katika vituo mbalimbali vya redio hivi sasa.Wimbo unaitwa Napenda Nini .Katika wimbo huu Jafarai ameshirikiana na mwanadada Fatma. Ni wimbo ambao una tungo kali,matata na ambayo nadhani ni huru kusema unaweza kuitafsiri unavyotaka wewe.Ni kazi nzuri ya sanaa ambayo inaonyesha jinsi gani lugha ya Kiswahili ni pana.Usikilize wimbo huo hapa chini na kisha jiulize; Jafarai Anapenda Nini?