BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Sunday, March 6, 2011

SHOW YA ROMA FUNIKO BOVU TANGA!!

Ile show ya msanii nguli wa hip hop kutokea Tanga R.O.M.A iliyofanyika kunako Club Lacasa Chica imekuwa gumzo jijini hapa baada ya msanii huyo kuzikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kiwango cha juu. Show hiyo iliyopewa jina la NARUDI NYUMBANI PARTY, ilisindikizwa na wasanii wengine kama Belle 9 pamoja na Young D ambao nao walitoa burudani ya hali ya juu.

Roma akiwarusha wakazi wa jiji la Tanga alipokuja kuwashukuru kwa kumfikisha alipo sasa.

Warembo wa kitongoji cha Miss Central walikuwepo na walipita kuwasalimia mashabiki.

Msanii Belle 9 akiimba jukwaani kwa hisia kali kuhakikisha anawapa burudani mashabiki wake.

Mc wa show alikuwa Rass Bizzle kutoka Nyakubi Inc....

Vijana wa Town Boys walikuwepo. Na hapa kitu cha kiduku pale kati.

Jha, jha, jha.....Tayana alikuwepo. Kaa tayari, video za show nzima inakuja.


No comments:

Post a Comment