Warembo wa kitongoji cha Miss Tanga City Central wakiwa katika mazoezi kunako klabu Pweza iliyopo chuda relini. Kitongoji hicho ambacho ndio kimefungua pazia la mazoezi jijini hapa, kimejitapa kutoa mshindi kwa mwaka huu. Mbio za mashindano ya kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 zimeanza hivi karibuni huku taji hilo likishikiwa na Anna Kiwambo ambaye ni Miss Tanga 210. Miss Tanga 2011 inaandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment.


No comments:
Post a Comment