BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, March 1, 2011

ROMA/BELLE 9/ KUWASHA MOTO JIJINI TANGA IJUMAA HII!


Msanii wa Kizazi kipya Ibrahim Mussa a.k.a Roma anatarajia kuwasha moto mjini Tanga kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuweza kumuunga mkono katika kazi yake ya sanaa ambayo amekuwa akiifanya.

Akizungumza na blog hii, mratibu wa tamasha hilo lililopewa jina la 'Narudi Nyumbani Tanga, Bw. Nickson Amos alisema kuwa litafanyika katika ukumbi wa La Gland la Casa chica Ijumaa ya tarehe 4.03.2011.

"Kweli Roma atafanya tamasha lake binafsi ambalo anatarajia kusindikizwa na Belle 9 na Young D hivyo wakazi wa Tanga waje kwa wingi kumuunga mkono.

Aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo kuwashukuru wakazi wa Tanga kwa kuweza kumuunga mkono tokea ameanza kazi zake.

No comments:

Post a Comment