BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, March 22, 2011

MASHINDANO YA SHIMIWI NI OKTOBA JIJINI TANGA

MASHINDANO ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) mwaka 2011 yamepangwa kuanza Oktoba 13 hadi 30 Tanga. Akizungumza na Blog hii, Katibu Mkuu wa Shimiwi, Ramadhani Sululu alisema michezo hiyo ya kila mwaka inashirikisha wanamichezo wanawake kwa wanaume.

Alisema michezo tisa itashindaniwa katika mashindano hayo ambayo mwaka jana hayakufanyika kutokana na Uchaguzi Mkuu. Alitaja michezo itakayoshindaniwa kuwa ni soka na vishale ambayo itashindanisha timu za wanaume na netiboli wanawake.

Michezo ambayo itashindaniwa na wanaume na wanawake ni kuvuta kamba, riadha, bao, karata, drafti na mbio za baiskeli. Shirikisho hilo limeomba viongozi wa klabu za michezo kuwapa umuhimu wa kwanza walemavu ambao wanauwezo wa kushiriki michezo hiyo.

“Tunaomba kama kuna watu wenye ulemavu ambao wanauwezo wa kushiriki kati ya michezo itakayoshindaniwa wapewe kipaumbele katika uteuzi wa timu,” alisema. Sululu alisisitiza klabu zote wanachama kuthibitisha michezo watakayoshiriki hadi Septemba 30 na kufika Tanga siku moja kabla ya mashindano kuanza.

Katibu huyo pia aliwakumbusha wanachama kulipa ada ya mwaka Sh 600,000 na 400,000 ya ushiriki kwa wakati kabla ya Septemba 30. Wakati huohuo Sululu alisema Mkutano Mkuu wa Shimiwi uliokuwa umepangwa mwezi huu umesogezwa mbele hadi baada ya mashindano ya Shimiwi.


Na: Anna Makange, Tanga

No comments:

Post a Comment