Akiongea mmoja wa waratibu wa onyesho hilo alisema madhumuni halisi ni ya onyesho hilo ni kuwaleta karibu wanachuo wote kwa pamoja ambao kwa muda mrefu walikuwa likizo pamoja na kuwapa burudani ya kutosha.
“Unajuwa walikuwa likizo ndefu kabisa na juzi juzi tu ndio wamefungua vyuo kwahiyo ni katika utaratibu wa kawaida kabisa wa Str8 Muzik kuwaleta karibu wanachuo hao na pia kuwapa burudani ya kutosha, zaidi ya D’Banj wengine watakaopamba jukwaa ni kutoka nchini Kenya Nonini,Jua Cali, wakati Tanzania atakuwepo TID, Mangwea, na wengine wengi” alisema mratibu huyo.
Katika onyesho hilo ambapo kutakuwa na usafiri wa wanavyuo kwenda na kurudi uwanjani kiingilio ni Tsh 3,500/- tu.
No comments:
Post a Comment