Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya dunia, mrembo atakayefanikiwa kuibuka mshindi katika taji hilo la mavazi ya ufukweni anakuwa tayari amepata tiketi ya kuingia katika hatua ya 20 Bora ya shindano kubwa la kumtafuta malkia wa dunia.
Lundenga alisema kuwa hiyo ni moja ya mafanikio kwa mwakilishi huyo wa nchi kwa sababu ameonekana kuwa ni bora katika vazi hilo.
Alisema pia wanaomba Miriam aendelee kufanya vizuri leo na kupata nafasi ya kuingia hatua ya 20 Bora ya fainali ya mashindano hayo ambayo imepangwa kufanyika Desemba 12 katika jiji la Johannesburg.
Alisema kuwa warembo wote wanaoshinda katika mataji madogo madogo, wanaingia moja kwa moja kwenye hatua hiyo ya 20 Bora ambayo inakuwa rahisi zaidi kushinda taji la Miss World.
Mrembo mwingine aliyeingia katika hatua ya 20 Bora ya mashindano hayo ni kutoka Japan ambaye aliibuka kidedea katika taji la michezo. Mrembo huyo ambaye aliwahi kushiriki katika michuano ya Olimpiki, aliwashinda wenzake katika mbio fupi.
Warembo hao pia walishindana katika kupiga penati.
No comments:
Post a Comment