BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Saturday, November 14, 2009

MH TEMBA, CHEGGE KUPIGA SHOW DUBAI

Machizi wanaoifanya TMK Wanaume Family iwe juu kwa sasa, Amani James Temba ‘Mheshimiwa’ na Said Juma ‘Chegge’ wanatarajiwa kudondoka pande za Dubai na kufanya shoo ya ukweli.

Chegge na Mh. Temba watakuwa Dubai ambapo jukumu lao ni kutoa shoo zitakazofanyika Mwezi huu, mwaka huu lakini Novemba 21 watakuwa Dar na kufanya vitu vikali na kuinogesha Fiesta 2009.

Temba amesema kuwa kila kitu kipo confirmed na kwamba tayari wameshaanza maandalizi ya kupiga shoo hiyo ambayo wamekwishavuta mzigo nusu.


Mbali na hilo, kupitia hapa unaweza kupewa information kuwa video ya wimbo Running Low ya Wahu ambaye ni mtoto wa Kenya na Chegge a.k.a Mtoto wa Mama Said siku chache zijazo itakuwa kideoni.


No comments:

Post a Comment