BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, November 7, 2009

MPIGIE KURA ELIZABETH ILI UMUOKOE KWENYE JUMBA LA BBA



Africa nameingia kwenye ‘Danger zone’ baada ya kuwekwa ndani ya mchujo,
kitendo kinachoashiria huenda akaaga Jumba la BBA wiki hii (Jumapili).
Eliza ameingia ndani ya mchujo baada ya mkubwa wa jumba wiki hii,
Edward kumuokoa rafiki yake kipenzi na mvuta sigara mwenzake Mzamo,
ambaye alikuwa kwenye orodha ya mstari mwekundu.

Big Brother aliwatangaza washiriki waliopigiwa kura wiki hii na kuingia
kwenye mchujo kuwa ni Nkenna, Emma aliyenusurika kutoka wiki iliyopita
na Mzamo ambaye ameokolewa na rafiki yake.

Hali ilibadilika pale Edward alipoitwa katika chumba cha mahojiano na
Big Brother na kuulizwa ni nani anayetaka kumuokoa, bila kusita
alimtaja rafiki yake Mzamo na kumweka Elizabeth aondoke badala yake.
Kwa hatua hiyo, huenda Eliza akaaga Jumba la BBA wiki hii. Ili
kumuokoa, mpigie kura kwa wingi ili aendelee kutesa na mwisho wa siku
aibuke na ushindi.
Mpige kura Eliza kwa kuandika jina lake (VOTE ELIZABETH) kisha kutuma
kwenda namba 15726.




No comments:

Post a Comment