BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, November 17, 2009

MISS UTALII 2009 TANGA- NANI KUIBUKA MNYANGE..??
Shindano la kumsaka mnyange wa Miss Utalii 2009 jijini Tanga linzaidi
kupamba moto huku kila mshiriki akipania kuibuka kidedea. Shindano hilo
lililo na dhana ya kutangaza utalii nchini Tanzania, linatarajia
kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 20 mwaka huu.

Katika pita pita za VIJIMAMBO VYA TANGA kunako baadhi ya mitaa ya
jijini hapa, tayari waaandaji wa mashindano hayo makubwa wameshabandika
matangazo kila kuna ili kuwapa watu habari kuhusu tukio hilo.

Shindano hilo ambalo linatarajiwa kushirikisha karibu warembo tisa,
litafanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort, hoteli mpya na yakisasa
mkoani Tanga iliyopo maeneo ya Sahare.

Kwa mujibu wa waandaji wa mashindano hayo ambao ni RAHA ENTERTAINMENT
pamoja na BREEZ FM RADIO,onyesho la miss utalii linatarajiwa kuanza
majira ya saa mbili usiku huku kiingilio kikiwa ni 25000.
Hata hivyo shindano hilo linatarajiwa pia kupambwa na burudani safi
kutoka wa Kassim, Maunda Zorro, Steve aliyewahi kutamba kwenye wimbo wa
Blue wa tabasamu pamoja na Price Mwinjuma Muumini akiwa na kundi zima
la Bwagamoyo International band lenye maskani yake jijini Tanga
Tanzania.

Pamoja na shindano hilo la Miss Utalii 2009 kuletwa na RAHA
ENTERTAINMENT NA BREEZ FM RADIO, lakini pia kuna wadhamini wengine
ambao ni Tanga Beach Resort, Aurora Security,Silvarado Hotel, Saska
Digital Lab, Tanga Middle Age Veterans.

Gari inayotumika kubebea warembo wa Miss Utalii jijini Tanga

Watangazi wa Breez Fm radio ya jijini Tanga ambao ni moja ya waandaji wa Miss Utalii Tanga, Ben aliyevaa shati jeupe na Tin Daddy mwenye fulana wakiwa kwenye Pozzz

Mkali wa milazo, Dj Bob Nass akiwa na Tin Daddy na Ben

No comments:

Post a Comment