BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Sunday, November 8, 2009

YOSSOU N’DOUR NA ANGELIQUE KIDJO KUFANYA ONYESHO NCHINI TANZANIA

Wasanii wakubwa kabisa barani Afrika na Ulimwenguni kote, Angelique Kidjo kutoka Benin na Yossou N’Dour wa Senegal, wanatarajia kufanya onyesho lao moja jijini Dar litakalofanyika katika viwanja vya Karimjee, Novemba 15 mwaka huu.

Wasanii hao ambao watatua hapa bongo kwa mwaliko mkubwa wa kampuni ya simu ya Zain Tanzania.

Meneja masoko wa kampuni hiyo Costantine Magavila alisema kuwa onesho hilo ni maalumu kwa wakazi wa Dar, pamoja na watumiaji wa mtandao wa Zain.

Magavila alisema kuwa wasanii hao watakuwa jukwaani kuanzia saa moja usiku hadi saa sita usiku na wanatarajia kuwasili nchini Novemba 13 mwaka huu tayari kwa onesho hilo.

Magavila alibainisha kuwa onesho hilo litatoa nafasi kwa watumiaji wa huduma ya ZAP, kupata punguzo la bei kuwashuhudia wasanii hao ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo watalipia sh 20,000/= badala ya sh. 25,000/= kama watu wa kawaida.

ENJOY VIJIMAMBO VYA TANGA

No comments:

Post a Comment