Akizungumza na Blog hii, msanii huyo amesema kuwa ngoma ya MR PRESIDENT ilimchukua muda hadi kuifanikisha toka alipotangaza kwani alishafanya kazi producer Duke wa M- Lab Record na ngoma kukamilika. Lakini hata hivyo msanii huyo aliahirisha kui'riliz ngoma hiyo na kuamua kufanya kazi na J Marder wa Tongwe Record iliyopo Masaki jijini Dar Es Salaam.
Mkali huyo wa Hip Hop kutokea Tanga, Tanzania ameongeza kuwa hadi sasa yupo Tongwe Record chini ya mmiliki wake J Marder na tayari kuna ngoma nyengine anazitayarisha kwa ajili ya kutoka na albamu hapo baadae.
Roma amewataja baadhi ya wasanii ambao anatarajia kuwapa shavu kwenye ngoma zake mpya ni pamoja na Izzo B na Nick Wa Pili ambazo ataziachia very soon.
Mchizi wangu wa ukweli alimalizia kuwa, bado yupo na YUDDI ambaye ni Mixing Producer wake aliyefanya ngoma ya TANZANIA. Mnoma alizitaja baadhi ya redio ambazo hadi sasa zinagonga ngoma yake kuwa ni Mwambao Fm ya Tanga, Breez Fm, Clouds Fm, Times Fm, E.A Radio, Coconut Fm, Magic Fm pia imefika Mtwara, tabora na karibu nchini nzima.
Dizaini mnoma kama amebanwa na skuli, bt amesema kuwa yupo mbioni katika mpango mzima wa albamu punde tu atapokuwa free.
No comments:
Post a Comment