BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, November 7, 2009

FID Q MKALI WA HIP HOP KUPITIA VIJIMAMBO VYA TANGA



Katika shindano lisilo rasmi la kumsaka mkali wa Hip Hop nchini Tanzania kupitia blog hii, limemalizika huku msanii Fid Q akiibuka kidedea.


Shindano hilo lililochukua takribani mwezi mmoja huku ikiruhusu mashabiki na wadau kupiga kura, lilikuwa likiwashindanisha Joh Makini, Langa, Prof Jay, Mabovu, Chid Benz pamoja na Fid Q aliyewafunika wenzake.




Fid Q, mwanamuziki machachari wa muziki wa kizazi kipya alifanyiwa mahojiano na jamaa wa Channel O. Kumbe jamaa wanamnyaka sana tu huyu mshikaji. Safi sana Fid

Prof Jay na Chid Benz walitoka sare kwa kupata kura 3, huku Joh Makini akipata kura 2- Mabovu alipata kura 1 wakati Langa aliambulia patupu. Ni Fid Q pekee ndie aliyeibuka na kura 5 zilizompa ushindi ambao sio rasmi kwa mujibu wa blog hiii. Anko Mo Blogspot imekuwa ikishindanisha wasanii ama kundi la muziki ili kuwapa chachu wadau wa VIJIMAMBO VYA TANGA waendelee kupata burudani. Asanteni wote mliopiga kura, endeleeni kuhabarika.

No comments:

Post a Comment