BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, December 1, 2010

LEO NI SIKU YA UKIMWI DUNIANI!!

Siku ya Ukimwi Duniani inakumbukwa kila tarehe moja Desemba. Hii ni siku maalum ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa Ukimwi. Desemba moja ilichaguliwa kuwa ni siku ya Ukimwi kutokana na tarehe hiyo kuwa ndio siku ambayo kirusi cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981. Toka mwaka 1981 watu zaidi ya milioni 25 wameshafariki kutokana na Ukimwi.

Siku hii ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. Kuanzia hapo siku hii imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanaharakati.

Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS ililipa shirika lisilo la kiserikali la Kampeni ya Ukimwi Duniani (the World AIDS Campaign) wajibu wa kuratibu siku hii.

Kila mwaka siku hii hukumbukwa kwa ujumbe maalum. Ujumbe wa mwaka 2005 ni Zuia Ukimwi: Timiza Ahadi. Ujumbe huu utatumika hadi mwaka huu wa 2010. KAPIME UJUE AFYA YAKO EWE MDAU MTANZANIA, EWE MDAU WA 'VIJIMAMBO VYA TANGA'!

No comments:

Post a Comment