BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, December 7, 2010

"WAPELEKWE SHULE WASOMA MITA"- MKAZI WA NGAMIANI

BAADHI ya wakazi wa Jiji la Tanga wameishauri Mamlaka ya Maji safi na Maji taka, kuwapeleka shule wasoma mita za maji, ili kuboresha utendaji wao.

Rai hiyo ilitolewa na mkazi wa Ngamiani, Hassan Tarimo, wakati wa mkutano wa pamoja na wadau wa mamlaka hiyo (EWURA) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma za maji, iliotolewa na mamlaka ya maji safi na maji taka Tanga.

“Ombi langu kubwa ni kuwa hawa wafanyakazi wanaosoma mita hawana utaalamu wa kutosha, hivyo basi tunauomba uongozi wa mamlaka kuwapeleka shule. Inavyoonyesha hawajui, kwani kila mwezi kunakua na tofauti kubwa ya bili wanazozileta,” alisema Tarimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Joshua Mgeyekwa, amekiri kuwepo kwa tatizo na kuongeza kuwa watakutana na meneja wa huduma kwa wateja ili waweze kumaliza kero hiyo.

Inadaiwa kwamba wasomaji wengi wa mita za maji hawana elimu ya kutosha ya kazi zao, kitu kinachosababisha wateja wao kuwa na bili zenye tofauti kubwa ya uwiano kwa kila mwezi.

Na Bertha Mwambela, Tanga

No comments:

Post a Comment