BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, December 6, 2010

SAFI MATONYA- UMETUWAKILISHA VYA KUTOSHA!

(Matonya na Davis ambaye pia ni mshindi wa Tusker Project Fame 4 wakiimba)

Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanga, Tanzania Matonya, jana alifanya show ya aina yake kunako mashindano ya Tusker Project Fame 4 wakati washiriki walipoimba na mastaa wa muziki ambao wanatambulika katika tasnia hiyo.

Matonya aliitwa baada ya mshiriki kutoka nchini Uganda anayejulikana kama Davis kuchagua kuimba na msanii huyo. Kwa pamoja waliimba nyimbo mbili za Matonya ambapo walifanya utambulisho wa Vaileti na muda kidogo wakaimba wimbo mwengine Anita. Hii ni heshima kubwa kwa msanii Matonya kuuwakilisha mkoa wa Tanga.

Hata hivyo katika hatua nyingine ya mashindano hayo Mtanzania pekee aliyeingia fainali hizo Peter Msechu aliweza kukamata nafasi ya pili huku Davis wa Uganda akiibuka mnyange.Enjoy 'Anita' ya Matonya hapa.

No comments:

Post a Comment