BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, December 15, 2010

UKARABATI UWANJA WA MKWAKWANI TANGA KUGHARIMU SHILINGI MILIONI 22!!

UWANJA wa soka wa Mkwakwani Jijini Tanga,ambao umfungwa kwa ajili ya
matengenezo unatazamiwa kufunguliwa rasmi Januari 10 mwakani baada ya
kukamilika kuwekwa nyasi katika sehemu ya kusakatia kabumbu.

Meneja wa uwanja huo,Mbwana Msumari alisema kuwa matengenezo
yanagharamiwa na kampuni ya Azam inayomiliki timu ya Azam FC na hadi
utakapokamilika kiasi cha sh 22 milioni zitakuwa zimetumika.

Alisema sehemu nyingine zinazofanyiwa matengenezo hayo zaidi ya
kupanda nyasi ni kufufua kisima,kuweka tiles katika vyoo kukarabati
mfumo wa umeme na kuweka mabenchi mapya kwa ajili ya kukalia
waamuzi,wachezaji wa akiba na waandishi wa habari.

“Hadi sasa upandaji nyasi katika pitch unakwenda vizuri kwa kuwa maji
ni mengi yanamwagiliwa masaa mengi”alisema Msumari na kumpongeza
mtaalamu wa upandaji nyasi Athumani Madenge kutoka klabu ya Azam FC.

Meneja huyo alisema utakapokamilika uwanja huo hautatumika kwa
shughuli nyingine zaidi ya soka na kwamba,matamasha yatakuwa
yakiendeshwa katika eneo la pili.

Afisa Utawala wa klabu ya Azam FC,Selemani Mabehewa alimfahamisha
mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kwa kushirikiana na CCM Mkoa
wa Tanga wamepanga kukamilisha kazi mapema ili kutoa nafasi ya timu
yake kuutumia uwanja huo katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Watumishi wa uwanja huo wa Mkwakwani walizungumza na mwandishi wa
habari hizi na kuipongeza Azam FC kwa kuamua kuukarabati uwanja huo
ambao ulikuwa katika hali mbaya.

No comments:

Post a Comment