Mkurugenzi wa shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA) la mjini Pangani, Dkt. Vera Pieroth alisema mjini huo wa kihistoria umetajwa kuwa ni miongoni mwa miji 93 ya urithi wa Utamaduni iliyopo katika nchi 47 duniani zinazotambuliwa na shirika hilo.
Vera alisema kuwa uamuzi wa kutunuku mji huo heshima hiyo umetangazwa hivi karibuni na Rais wa WMF, Bonnie Burnham, jijini New York, Marekani ambapo mji wa Pangani umekuwa kati ya maeneo manne katika bara la Afrika ambayo imepewa hadhi na WMF.
Miaka miwili iliyopita UZIKWASA kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya Kale iliendesha kongamano la kujadili jinsi ya kuhifadhi na kutanga Mali kale na urithi wa Utamaduni wa Pangani, lililofadhiliwa na Ubalozi wa Ujerumani na Wizara ya Maliasili na Utalii, na baadaye kufanyika utafiti wa kubainisha maeneo ya urithi wa utamaduni na historia yaliyopo katika Wilaya ya Pangani.
Kwa kutambuliwa na shirika la WMF lililoanzishwa mwaka 1965 kwa lengo la kuhifadhi, kutunza na kuendeleza maeneo ya makumbusho ya urithi wa Utamaduni na mali kale, mji wa Pangani sasa unatangazwa na kutambuliwa rasmi kuwa ni sehemu ya Utalii wa kihistoria na kiutamaduni Duniani.
No comments:
Post a Comment