
“Hii ni single ya kwanza,” alisema muimbaji huyo wa Bongofleva. “Nimesharekodi baadhi ya nyimbo na huu ni mwanzo tu.”
Muimbaji huyo amesema wimbo huo umerekodiwa katika studio ya B.Hitz ya prodyuza bora wa mwaka jana wa tuzo za Kili Hermy B na unamfafanulia mpenzi wake kwamba yeye ni mtulivu katika mahusiano yao.

K-Lyinn alisema wimbo huo ameuimba kwa lugha ya Kiingereza ingawa pia kiswahili kimo. Miongoni mwa mashairi katika wimbo huo yanasema: “Wanaume wananitolea macho lakini mimi ni wako, acha wivu.”

Muimbaji huyo anasema wakati fulani alipokuwa katika ziara zake za kimuziki nje ya Tanzania, alishaulizwa, “Huwezi kutuimbia kwa lugha tuijuayo?” “Ndio sababu nikaamua kutoka namna hii kivingine,” alisema muimbaji huyo aliyepotea kwa muda kwenye gemu ya muziki.
No comments:
Post a Comment