
Victoria Martine (20) na Juliet William (19) walichaguliwa kufuatia mchakato uliochukua takribani miezi mitatu huku ukiendeshwa na kamati maalum iliyochaguliwa na waandaaji wa Miss East Africa ambapo kamati hiyo ilikutana na warembo zaidi ya 150 kutoka sehemu mbalimbali Nchini ili kupata wawakilishi wawili wanaofaa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya urembo.
Victoria Martine, ni mrembo maarufu hapa Nchini ambae anajishughulisha na mambo ya mitindo, na pia amewahi kushinda tuzo ya reds fashion ambassador kwa mwaka 2007 Juliet William, yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha USIU cha jijini Nairobi, na pia ni mshindi wa tatu wa mashindano ya Miss Tanzania kwa mwaka huu.

Mashindano hayo yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam, na kudhaminiwa na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, CMC Automobile, na AKO Catering Services.
No comments:
Post a Comment