BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, December 18, 2009

NIMEWAKUMBUKA MASUDI KIPANYA NA FINA MANGO

Najua utakuwa unakifahamu kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na redio Clouds Fm iliyopo jijini Dar es salaam. Kipindi hiko kwa sasa kinafanywa na Babra Hasan na Gerlad Hando...ila hapo awali kilikuwa kikifanywa na Fina Mango pamoja na Masoud Kipanya.

Dah washkaji walikuwa juu sana, mlitufanya tuwahi kuamka kwa ajili yenu. binafsi nilikuwa napenda sana kuwasikiliza wanavyoleta raha na kuibua hisia zilizokuwa zimejificha.

Walikuwa wanaleta masihara penye ukweli, lakini wakijaribu kudadavua yale ambayo yana mguso katika jamii ili wasivunje sheria za nchini.

Kipindi kilikuwa kimesimama kweli- Masoud tunajua kazi zake ila najiuliza Fina yupo wapi na anafanya nini kwa sasa..?

Pamoja na hayo tunawakumbuka sana, mlikuwa wa kwanza kukaribishwa bungeni na mkarushwa live na Mh. Spika wa Bunge Samweli Sitta.
We Miss U Guys!!!


1 comment:

  1. Jombaa umenikumbusha mbali sana juu ya watu hawa enzi hizo bado niko scool nilikuwa nawambamba mara moja moja sana ila nikuwa nawa fell mbaya

    ReplyDelete