BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, December 14, 2009

Q CHILLAH NA TID WASHIKANA UCHAWI (PART 1)

The Big Names katika Bongo Flava nchini, Shabani Katwilla ‘Q-Chief’ na Khaleed Mohamed ‘Tid’ hivi karibuni wametoleana maneno ya kashfa kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa ni mchawi.

Ishu nzima iko hiviiii...juzi kati jijini Dsm, mtangazaji mmoja wa kike wa kituo kimoja cha televisheni aligonga mbili tatu hewani na msanii Q-Chief.

Wakiwa kwenye mahojiano ya laivu, Q-Chilah alisikika akisema kuwa tangu ameacha kufanya kazi na TID mambo yake yamekuwa hayaendi vizuri na kwamba tatizo hilo limekuwa ni la kudumu kwa upande wake.Q-Chief aliendelea kusema siku moja akiwa katika mishemishe zake alikutana na mama mmoja (hakumtaja jina) aliyemwambia kuwa amelogwa na wasanii wenzake wawili akiwemo TID.


Q-Chief aliendelea kupigia msumari na kusisitiza kuwa, ni kweli amelogwa na wasanii hao na hakuna ubishi.


Kwa upande wa TID alisema kuwa, kauli ya Chilah imemdhalilisha sana hivyo ameamua kwenda kuripoti polisi na kwamba atahakikisha anamshughulikia kadiri ya uwezo wake.

No comments:

Post a Comment