BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, December 14, 2009

NI KINGS AND QUEENS YA AMBWENE YESAYAH

Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava, kijana Ambwene Yesaya ametoka tena, safari hii kasimama wima na mrembo Jokate Mwegelo kunako Kings and Queens yakiwa ni mapinduzi mengine kunako sanaa yake, pia ni maandalizi ya kuufunga mwaka 2009 na kuufungua 2010.

Akilonga muda baada ya kudondoka Bongo akitokea pande za Kenya, alikokwenda kukamilisha mchongo wa pini hilo mchizi alisema kwamba ngoma ya Kings and Queens itatoka kwa staili ya video na kwamba kabla ya kusambaa kwenye runinga za TZ itaanza kuonekana MTV.

“Mbali na video hiyo ambayo nimeigonga Kenya kupitia Kampuni ya Ogopa pia kwa upande wa redio nimeachia kazi nyingine yenye jina la Bed and Breakfast ambayo imeifanyika ndani ya studio za B. Hitz Music Group chini ya Prodyuza Hermy B,” alisema A.Y.

Kitu kingine kipya alichosema Ambwene ni kwamba, kazi hiyo imefanyiwa mautundu zaidi (Mastering) katika studio za Ogopa Deejays. “Siku chache zijazo natarajia kwenda kupiga video yake na Kampuni ya Film Online iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini. Nawashukuru sana fans wangu, msichoke kunisapogti, sitawaangusha,” alisema.


No comments:

Post a Comment