BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, December 30, 2010

FRIENDS OF TANGA GET TOGETHER PARTY 2010 NI KESHO!!!

Ukitaka kwenda POPOTE utafika POPOTE.....lakini ukitaka kwenda TANGA, ungana na MARAFIKI WA TANGA siku ya kesho ya tarehe 31/12/2010 katika FRIENDS OF TANGA GET TOGETHER PARTY 2010. Utembelee vivutio vya kitalii huku ukipata kujua mambo mbali mbali mapya yanayohusu mkoa wa TANGA.

Piga namba hii kwa kufanyiwa booking ya usafiri wa kuja TANGA kama upo DAR (0714434452) Kwa wageni wote watakaofika kesho, watapokewa vizuri. Piga namba (0719000010) uje upokewe na upelekwe mahala ambapo MARAFIKI WOTE WA TANGA WATAKAPOFIKIA!! Tumalize mwaka kwa kujenga URAFIKI!

Wednesday, December 29, 2010

MBWELA CHIFU WA KWANZA WA WAZIGUA KUTIA SAINI MKATABA NA DK. KARL PETERS

Dk. Karl Peters (kati) akiwa na wenzake Dk. Karl Juhlke na Joachim Graf. Huyu Dk. Karl Peters ndiye aliyewaingiza mkenge babu zetu wakati wa kuingia ukoloni wa Ujerumani nchini kwa kuingia katika mikataba ya kilaghai na watawala wetu wa jadi.

(Mbwela, Chifu wa Wazigua mkoani Tanga, ndiye aliyekuwa mtawala wa jadi wa kwanza kutia saini mkataba na Dk. Karl Peters mwaka 1884.)

Haya na mengi mengineyo yanayohusu historia ya nchi hii yanapatikana katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar ambako kwa sasa ukarabati wake unakaribia tamati ili kuifanya sehemu hiyo isiwe tu ya makumbusho bali sehemu ya kukutania wadau wakubwa kwa watoto, wake kwa waume kwa shughuli mbalimbali ikiwemo utamaduni, sanaa na mengineyo.

Makumbusho hiyo ya Dar (katikati ya jiji karibu na IFM na sio Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama kama ambavyo wengi wamezoea kuchanganya) hivi sasa inajulikana kama Makumbusho na Jumba la Utamaduni - Museum and House of Culture.

Thursday, December 23, 2010

MERRY X-MASS AND HAPPY NEW YEAR 2011 WADAU!!

TUWAKUMBUKE MASHUJAA WETU WA TANGA!

Bwana Heri bin Juma (pia: bana Heri) alikuwa sultani wa Saadani iliyokuwa bandari ya biashara kwenye mwambao wa Bahari Hindi katika Tanzania kaskazini-mashariki tangu miaka ya 1870.

Mtawala wa Saadani

Alitawala chini ya Sultani wa Zanzibar kama mkubwa wake lakini akafaulu kutetea nafasi yake kama sultani aliejitegemea. 1882 aliweza kushinda jeshi la Sultani Sayyid Bargash aliyetaka kutawala Saadani moja kwa moja. Saadani kama miji mingine ya pwani ilifaidika na biashara ya Wazungu walioleta bidhaa na kulipa ushuru. Alielewana vema nao.

Kuja kwa Wajerumani

1886 Sultani Sayyid Khalifa wa Zanzibar alikodi eneo lake katika Tanganyika bara kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki. Bwana Heri pamoja na viongozi wengine aliona amesalitiwa na Sultani hakuwa tayari kukubali utawala wa Wajerumani. 1888

Vita ya Abushiri

Bwana Heri aliunga mkono na upinzani wa Abushiri dhidi ya Wajerumani akipata usaidizi wa makabila wa eneo lake hasa Wazigua.

Alishambuliwa na kiongozi Mjerumani Hermann von Wissmann aliyekuwa na silaha za kisasa akapaswa kuacha kambi yake Saadani tar. 6 Juni 1889. Aliendela na vita ya msituni. Baada ya kushambuliwa tena na jeshi la Wajerumani katika Januari na Machi 1890 uwezo wake ulikwisha. Sayyid Khalifa aliwasiliana naye na Wissmann akatayarisha kujisalimisha kwake tar. 6 Aprili 1890. Wissmann aliyemheshimu Bwana Heri hakumwua kama Abushiri bali akamwambia kujenga Saadani upya.

Upinzani wa wenyeji ulishindwa lakini ulisababisha mwisho wa utawala wa kampuni iliyoshindwa kukandamiza uasi wa Waafrika. Serikali ya Ujerumani iliona haja ya kungilia kati na kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mkononi mwaka kama koloni ya serikali ya Ujerumani.

Mwisho wake

Mwaka 1894 alijaribu tena kupambana na Wajerumani lakini alishindwa kwa mara ya pili. Akaondoka bara kwenda Zanzibar alipokufa baadaye.


Wednesday, December 22, 2010

WANAOVUMA KUTOKA TANGA!!

Asmah Makau- mkurugenzi mtendaji wa Five Brothers Entertainment na pia ni mfanyakazi wa Clouds Media upande wa Radio akiwa anatangaza kipindi cha JAHAZI sambamba na Kibonde na Regina.

Aisha Kisoky ni mbunifu wa mavazi, ambaye analimiki kampuni yake ya mavazi ya KOKOLIKO MODEL. Lakini pia ni mmiliki wa SOFIA PRODUCTION

Antonio Nugas a.k.a SWAHIBA ni mtangazaji wa Cloud Tv kupitia kipindi cha KAMBI POPOTE

VERONICA ANAWATAKIA HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA WA 2011

Veronica Stima wa AARSLEF BAM INTERNATIONAL anawatakia heri ya xmass na mwaka mpya 2011 familia yake ikiwa Tabora pamoja na wafanyakazi wote wa AARSLEF Dar es salaam,Iringa na Sumbawanga.Bila kumsaha Esther Ulaya,Joseph Stima na Cathbert Angelo wakiwa Dar es salaam.

Tuesday, December 21, 2010

PANGANI YATAJWA KUWA MOJA YA KIVUTIO CHA UTALII DUNIANI!

SHIRIKA la Makumbusho Duniani la World Monuments Fund (WMF) limeutambua na kuupa heshima mji wa Pangani kuwa mmoja wa miji mikongwe ya kihistoria na urithi wa Utamaduni duniani.

Mkurugenzi wa shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA) la mjini Pangani, Dkt. Vera Pieroth alisema mjini huo wa kihistoria umetajwa kuwa ni miongoni mwa miji 93 ya urithi wa Utamaduni iliyopo katika nchi 47 duniani zinazotambuliwa na shirika hilo.

Vera alisema kuwa uamuzi wa kutunuku mji huo heshima hiyo umetangazwa hivi karibuni na Rais wa WMF, Bonnie Burnham, jijini New York, Marekani ambapo mji wa Pangani umekuwa kati ya maeneo manne katika bara la Afrika ambayo imepewa hadhi na WMF.

“Kuteuliwa kwa mji wa Pangani ni faraja kubwa kwa watu wa hapa na shirika letu la UZIKWASA. Tangu mwaka 2007 shirika letu kwa kushirikia na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Kamati za kijamii tumekuwa kutangaza vivutio vya kihistoria vya mji hapa na tunafurahi sasa juhudi za pamoja ambazo zimeleta matunda mazuri,” alisema.

Miaka miwili iliyopita UZIKWASA kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya Kale iliendesha kongamano la kujadili jinsi ya kuhifadhi na kutanga Mali kale na urithi wa Utamaduni wa Pangani, lililofadhiliwa na Ubalozi wa Ujerumani na Wizara ya Maliasili na Utalii, na baadaye kufanyika utafiti wa kubainisha maeneo ya urithi wa utamaduni na historia yaliyopo katika Wilaya ya Pangani.

“Utafiti ulitusaibia kubainisha mambo mbalimbali, wananchi wengi walishiriki katika kutaja maeneo muhimu, kuibua vitu vya kizamani, kutoa picha na michoro, vyombo na mambo mengine mbalimbali ya kihitoria ambayo tuliyaweka kumbukumbu ambazo baada ya kupata baraka za Wilaya tulituma WMF na hatimaye tumepata heshima hii,” anasema.

Kwa kutambuliwa na shirika la WMF lililoanzishwa mwaka 1965 kwa lengo la kuhifadhi, kutunza na kuendeleza maeneo ya makumbusho ya urithi wa Utamaduni na mali kale, mji wa Pangani sasa unatangazwa na kutambuliwa rasmi kuwa ni sehemu ya Utalii wa kihistoria na kiutamaduni Duniani.

Monday, December 20, 2010

AT NA GELLY WA RYMES WALIVYOWASHA MOTO JIJINI TANGA!!

AT akiwa jukwaani akiwapa burudani wakazi wa jiji la Tanga katika show yake sambamba na Gelly Wa Rymes iliyofanyika kunako ukumbi wa Fax Night Club, show iliyoandaliwa na redio Breeze Fm ya jijini hapa.

Gelly akikonga nyoyo za mashabiki wake waliohudhuria kwenye show.

Mashabiki wakijirusha vilivyo wakati At na Gelly walipokuwa jukwaani.

Dj Bob Nass mwenye fulana nyekundu pamoja na Amirado, wote ni wafanyakazi wa redio Breez Fm iliyoandaa show.

Halaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Mashabiki

AT na Gelly walipokuwa redio Breez katika mahojiano kabla ya show.

Hapa ilikuwa one to one na mtangazaji.



Friday, December 17, 2010

ALLICE ANAWATAKIA HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA WA 2011

Administrator kutoka MARAFIKI WA TANGA Allice Joe Mkwabi anawataki Heri ya X-Mass na Mwaka Mpya. Ukitaka kutuma salam za X-Mass na Mwaka Mpya tuma picha yako kupitia (ankomo25@yahoo.com)


MERRY X-MASS WADAU- FURAHIA TOM & JERRY

X-MASS NJEMA

MARRY X-MASS WADAU WA VIJIMAMBO VYA TANGA

DIYANA ANAWATAKIA HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA!

Administrator kutoka MARAFIKI WA TANGA Diyana Ernest nae anawatakia wadau wa VIJIMAMBO VYA TANGA heri ya X-Mass na Mwaka Mpya.

ANAWATAKIA HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA!

Meneja wa kundi la Tip Top Connection Hamisi Shabani "Taletale" anawatakia wadau wa VIJIMAMBO VYA TANGA heri ya X-Mass na Mwaka Mpya. Una picha na unataka kutoa salam za X-Mass na Mwaka Mpya. Nitumie kupitia (ankomo25@yahoo.com)

MARAFIKI WA TANGA KUKUTANA DAR SIKU YA JUMAMOSI!!

MARAFIKI WA TANGA inakualika MBALAMWEZI BEACH CLUB jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kukutana na marafiki wenzako. Ni siku ya kesho Jumamosi ya tarehe 18/12/2010 kuanzia saa kumi na moja jioni, njoo ujionee ustaarabu wa MARAFIKI WA TANGA.

Kama wewe ni mtu wa TANGA na upo Dar, au sehemu nyengine yeyote. Hii ndio nafasi yako ya kukutana na MARAFIKI WA TANGA. Hata wale ambao sio watanga pia mnakaribishwa tufurahi kwa pamoja. Tujuze kama utafika kupitia (marafikitanga@yahoo.com)

BONYEZA HAPA KUKUTANA NA MARAFIKI WA TANGA





Thursday, December 16, 2010

IJUMAA HII NDANI YA TANGA NI GELLY WA RYMES NA AT!!

Wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava nchini At pamoja na Gelly Wa Rymes wanatarajiwa kufanya show ya aina yake siku ya Ijumaa ya tarehe 17/12/2010 kunako Club ya Fax Night iliyopo jijini Tanga.



Show hiyo ambayo pia itaongozwa na wasanii wengine kutoka Tanga, imeandaliwa na kituo cha redio Breeze Fm kinachorusha matangazo yake jijini hapa kwa masafa ya 100.6 fm.

Wednesday, December 15, 2010

UKARABATI UWANJA WA MKWAKWANI TANGA KUGHARIMU SHILINGI MILIONI 22!!

UWANJA wa soka wa Mkwakwani Jijini Tanga,ambao umfungwa kwa ajili ya
matengenezo unatazamiwa kufunguliwa rasmi Januari 10 mwakani baada ya
kukamilika kuwekwa nyasi katika sehemu ya kusakatia kabumbu.

Meneja wa uwanja huo,Mbwana Msumari alisema kuwa matengenezo
yanagharamiwa na kampuni ya Azam inayomiliki timu ya Azam FC na hadi
utakapokamilika kiasi cha sh 22 milioni zitakuwa zimetumika.

Alisema sehemu nyingine zinazofanyiwa matengenezo hayo zaidi ya
kupanda nyasi ni kufufua kisima,kuweka tiles katika vyoo kukarabati
mfumo wa umeme na kuweka mabenchi mapya kwa ajili ya kukalia
waamuzi,wachezaji wa akiba na waandishi wa habari.

“Hadi sasa upandaji nyasi katika pitch unakwenda vizuri kwa kuwa maji
ni mengi yanamwagiliwa masaa mengi”alisema Msumari na kumpongeza
mtaalamu wa upandaji nyasi Athumani Madenge kutoka klabu ya Azam FC.

Meneja huyo alisema utakapokamilika uwanja huo hautatumika kwa
shughuli nyingine zaidi ya soka na kwamba,matamasha yatakuwa
yakiendeshwa katika eneo la pili.

Afisa Utawala wa klabu ya Azam FC,Selemani Mabehewa alimfahamisha
mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kwa kushirikiana na CCM Mkoa
wa Tanga wamepanga kukamilisha kazi mapema ili kutoa nafasi ya timu
yake kuutumia uwanja huo katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Watumishi wa uwanja huo wa Mkwakwani walizungumza na mwandishi wa
habari hizi na kuipongeza Azam FC kwa kuamua kuukarabati uwanja huo
ambao ulikuwa katika hali mbaya.

ROMA, SAM WA UKWELI NA CYRIL KUFUNGA MWAKA PAMOJA!

Msanii mkali wa Hip Hop kutoka Tanga, Tanzania anayefanya vizuri kunako game ya Bongo Flava Roma. Anatarajia kufanya show sambamba na wasanii wengine wa muziki huo ambao ni Sam wa Ukweli pamoja na Cyril siku ya Jumamosi ya tarehe 18 kwenye ukimbi wa Dar West Park maeneo ya Tabata.

Show itakuwa ya FUNGA MWAKA, ikiongozwa na Adam Mchomvu kutoka Clouds Fm kwa kiingilio cha 5000/=. Fanya kama tunakutana pande hizo.

MFAHAMU KING MAJUTO WA TANGA!

Amri Athuman' King Majuto' alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini Jijini Tanga, alianza kuigiza 1958 kuigiza akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majato ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.

Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.

Monday, December 13, 2010

MARAFIKI WA TANGA INAZIDI KUPANUA WIGO!!

Kama wewe una account ya facebook basi itakuwa rahisi kwako kujiunga na mtandao wa MARAFIKI WA TANGA ambao unazidi kukua kila kukicha. Hapo unakutana na marafiki kutoka Tanga na nje ya Tanga na kubadilishana mawazo. Kuna Chat Room ambayo ni raha tupu....MARAFIKI WA TANGA sasa wana ID Card ili kuhakikisha Group hii inafika mbali zaidi. Pichani ni Sophia Murra ambaye pia ni member wa MARAFIKI WA TANGA. Group ina zaidi ya watu 200 hadi sasa.

Kijana Mussa Mhina, pia ni memebr wa MARAFIKI WA TANGA.

Dada Mariam Chuku Semfuko, ni miongoni mwa akina dada mahiri kutoka Tanga. Nae ni member wa MARAFIKI WA TANGA

Tanga Raha!! Eric John Mgondah, member wa MARAFIKI WA TANGA

Dada Fatma Olotu.....member wa MARAFIKI WA TANGA

Dj na Mtangazaji wa Breeze Fm Radio ya jijini Tanga- Nasr Thabit maarufu kama Dj Bob Nass nae ni member wa MARAFIKI WA TANGA

Kitojo Ever......kutoka MARAFIKI WA TANGA! Hawa ni baadhi tu ya members wa MARAFIKI WA TANGA ambao Group yake ipo facebook. BONYEZA HAPA KUKUTANA NA MARAFIKI WA TANGA



Sunday, December 12, 2010

Wednesday, December 8, 2010

TANGA TOWN LEO ASUBUHI!!

Eneo la stendi, njia ya kutokea kwa magari ya mikoani

Kituo cha kuwekea mafuta karibu na barabara ya 13

Tuesday, December 7, 2010

ROMA- SHUKRANI ZAKE ZA DHATI.

2010 ndiyo hiyo inakwisha…asante Mungu kwa kutupa pumzi yako hadi sasa, tunakuomba uwarehemu na kuwapumzisha kwa amani wale wote waliotangulia mbele ya haki (KIDOLE CHA MWISHO JUU )….AMEEN….
Napenda kutumia nafasi hii kufanya hiki ambacho pengine sikuwahi kukifanya kwa njia hii hapo kabla…..
ASANTE SANA CLOUDS .FM, KWA MCHANGO WENU MKUBWA KATIKA MZIKI NA MAISHA YANGU KWA UJUMLA…. HAPPY BE LATED BIRTH DAY NA MUNGU AWABARIKI SANA….WOTE WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO….sitaweza kuwataja wote, but kwa niaba ya hawa nitakaowataja watawakilisha wengine…

ADAM MCHOMV.…braza u knw wea we from…thanx sana kwa sapoti yako mzaz…nakumbuka wewe ni mtu wa kwanza kukukabidhi ngoma yangu ya 1(TANZANIA)ilikuwa kitega uchumi jumapili kwenye total request…ukaitambulisha kama suprize kwenye hot 3 siku ya jumanne…hahahahaha sitaisahau siku hii, nakumbuka ulimwambia fetty na b12 (kwa sasa anajiita navigator) wasikilize neno baada ya neno ktk ngoma hiyo…na huo ndo ukawa mwanzo wa ROMA hadi leo tunapeana support, thanx bro na Mungu akubariki sana mwanangu.

B..TWELVE…twangala twizzy una nafasi kubwa sana kwenye mziki wangu…u knw it son..wewe ni mtu wa kwanza mimi kukupa kazi zangu za ki – underground… hahahahaha daah zamani kidogo, nakumbuka 1st tym tunamit nakukimbilia kwenye bus alfajiri ukitoka tanga, mi nilikuwa nimetoroka shule (hostel), nikakukabidhi track zangu huku abiria wananishangaa ninavyokwambia, dizain oyaaa bro ndo ngoma zangu hizi uskize, aaf unambie zipoje!! hahahahaha hadi bus likaenda kunishusha mbele kabisa huko, nikarudi shule kwa mguu...nikiwa na imani zile ngoma zingenitoa but hata sijui ziliishia wapi hata sikuzisikiaga…nway sikukata tamaa, na leo umenifanya niwe ROMA… I do apriciate u son GOD BLESS U…n thanx 4everythin…

DJ…FETTY… mdomo wako umeonekana una Baraka sana, kwani kila ngoma yangu uliyoitambulisha kwa kinywa chako, ilifika mbali…mr..president…pastor…mechi za ugenini…BILA WEWE NISINGEFIKA HAPA PENGINE nakuheshimu sana…unanitendea haki…lakini niseme neno gani kumaanisha wewe ni muhimu kwangu? Ni jibu gumu kulipata…fetty mungu akupe maisha marefu yenye heri na fanaka…sauti yako imenifikisha mbali sana trust mi…mmwaaa lav u sister…

NCHA KALI…hahahahaha daaah bro mi siongei chochote kwako, zaidi ya hiki…WEWE NI “R” katika “R”oma…”R”UBEN… najua unajua ninachomaanisha bro…wewe ni zaidi ya WOTE…ulinitabiria mengi na sasa nayaona yanatimia….kila ninapotaka kufeli ukitia neno lako tu najikuta nafaulu…am countin on u always son…luv u

MULLY B & ARNOD KAYANDA….mully b thanx sana jamaa…kwa muvments zote tunazofanya…nakumbuka sana msemo wako dat SHOW THEM THEY HV 2PAY U…hahaha naliona hilo nw, limetimia coz nililifanyia kazi sana…thanx again….mwanangu kayanda miili yetu inafanana sana, but nasisi tutanenepa siku 1, hahahahaha am kidin u knw…support yako inaonekana sana kwangu..nathamini mchango wako mzazi usichoke kuninyoosha pale ninapopinda, happy birth day clouds fm again….

DJ..STEVE B….naithamini mno mikono yako, inanifanya nisikike na kujulikana mbali sana, huwa najisikia furaha mno unapopiga ngoma yangu au ngoma yoyote kali..nafurahi tunavyoishi poa nawe…unanifundisha mengi na naahidi kuyafanyia kazi…am nothing without u… still nahitaji support yako son….we go harder!!!!!

SUKA…..muda mwingi nisingefata unachoniambiaga pengine nisingekuwa hapa nilipo…basi naahidi nitaendelea kuyatenda yale unayoniambia…..itz obviously u always stand 4mi…n a promice u, a wont lechu down jombaaa….

GADNA & KIBONDE…challenges zenu zinanijenga sana…na najifunza mengi kupitia ninyi..asanteni sana brazaz….Mungu awaongezee pale mlipopungukiwa…ameeen
BABRA HASSAN….umenifanya nijulikane na wabunge, mawaziri na viongozi wakubwa, maana wengi husikiliza kipindi chako (POWER BREAK FAST) thanx sana…bila kumuacha braza GERALD HANDO na BONGE pia, mchango wenu nauapriciate mno, unanijenga haswaa kisanii na Napata x- posure ya kutosha, kupitia nyie....sina cha kuwalipa….Mungu awabariki mno…

DINNA & GEA….hahahahaha mashosti hao……asanteni sana kwa mchango wenu…mnapotaja jina ROMA tu, inakuwa ina nguvu (impact) sana kuliko wengine, maana kundi linalowasikiliza ninyi nalihitaji sana kwenye mziki wangu, hahahahaha ipo dip sana hii…kazi njema bana ndugu zangu…..

ANTONIO NUGAZ…..tanga moja mwanangu uwongo? Mungu kaumba hajaumba??? hahahaha pamoja mwanangu, tumetoka mbali unalijua hili, tu majirani wema sie atii…asante kwa support yako ubarikiwe sana…..

SUDDY BROWN….sasa wewe sasa daaah!!! sijui nisemeje,… hebu nisaidie…..toka nilipokufahamu sijawahi kujutia kukufahamu huko....wewe ni kila kitu kwangu, kwani huanzia kupitia kwako, ndo huwafikia wengine hao, hahaha u knw wat I min? Piga kimya…. thanx sana mwanangu suddy…. soory pia coz nakufelishaga sana unajua hilo, siko perfect bana u knw men….
SHADEE…..eee bi shosti huyo…tanga 1 mwanangu au siyo? Thanx daughter...pamoja sana 4 everythin vuvu…rrraaaaaaaah

DJ..BULLAH…mzaz a do apriciate u sana thanx 4 ol…kuanzia show yetu ya kat de luna fiesta…safi sana unanijulia ile ile mnyamwezi…pamoja bullah…mchango wako ni mkubwa pia especially dis fiesta 2010…thanx….

DJ…ARON…mzazi upo? Thanx too aron…tunapomit mara kwa mara tunakuwa na story tofauti na mziki…hii ni kwa sababu ya ukaribu na heshima tunayopeana thax son…unanisaidia mno braza….

DIVA & ZAMARADI…..zamaradi mketema…mi jina lako tu….hatucross sana na wewe bt pale inapotokea tu, hufanyika chochote kila kinachomake head line…hii inanikuza na kunijenga pia asante sana…lav ness lav…diva yoo…ajhajhajahjhajhajha…nini nitaongea kwako hadi watanzania wanielewe na harakati zangu hizi…?but mi ndo nafaham ukweli wa mchango wako kwangu…nasema shukrani mamaa….twende sawa tuu…..

BAGHDAD…..since agt to knw u…..2mekuwa 2kishauriana mengi mazuri yatupasa kuiendeleza hiyo hiyo nzuri pia…nakukubali sana kwa kile ufanyacho mwanangu na asante pia kwa msaada wako…kazi njema
JUMA DEREVA WA PRIME TIME…..wengi tuna msahau huyu mtu…ni mtu muhimu kwa wasanii wetu na wadau wengine pia bro unatusafirisha salama katika tour zetu, siku zote ulikuwa na una uwezo wa hata kututumbukiza kwenye uso wa semitrela, hahahhhhhaha hatuna budi kukushukuru asante sana juma…najua unanidai… ASANTE JUMA TUMEFIKA SALAMA ndo neno ninalokwambiaga kila mkoa tunaofika kwa show….

FAUZIA… uso wako mda wote umejawa na tabasamu zuuurii, kama moyo wako ulivyo mzuri, endelea hivo hivo dada angu, asante kwa kunilea vema…big boooos napenda kukuita hivo unalijua hilo…

SEBASTIAN MAGANGA…kabla sijatoka kimuziki, nilikuwa na drim nyingi nawe, ikiwemo kufanya inter view pa1, bt nw dayz hukikalii tena kile kiti...nway muda wowote niwapo nawe, nachukuaga mengi frm u, coz u genious son, thanx kwa kuniongelea vema….. hahahahaha nakuenjoy sana blaza…

P…JAY…mzazi nikikuona nakumbuka lile panga ulilolishika kule mkuranga hahahahaha unanikubali nami nakukubali pia…deuces…

RUGE & J.K….nguzo ya yote hayo niliyonena huko juu ni nyie…sifa zote za huko juu zianzie kwenu kwanza….God bless u …ol…

NAFURAHI TUNA KARIBIA KUUFUNGA MWAKA HUU 2010 NA KUANZA 2011…. MUNGU ATAKAPOJALIA…NAWATAKIA KILA LA KHERI WAFANYAKAZI WOTE WA KAMPUNI TAJWA HAPO JUU…NA WALE NILIOWASAHAU KUWATAJA SI KWA MAKUSUDI HAPANA, BALI NI MAPUNGUFU YA KIBINADAMU TUU...NISAMEHENI, BUT KAMA UNAWAKILISHA CLOUDS FM TU, NDO NIMESHAKUTAJA NO MATTER WAAAT
…HAPPY BE LATED BIRTH DAY AGAIN…..
DEUCES…..1
Katoliki “z ryt here…….TANGA ‘Z MA’ HOOD……..

"WAPELEKWE SHULE WASOMA MITA"- MKAZI WA NGAMIANI

BAADHI ya wakazi wa Jiji la Tanga wameishauri Mamlaka ya Maji safi na Maji taka, kuwapeleka shule wasoma mita za maji, ili kuboresha utendaji wao.

Rai hiyo ilitolewa na mkazi wa Ngamiani, Hassan Tarimo, wakati wa mkutano wa pamoja na wadau wa mamlaka hiyo (EWURA) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma za maji, iliotolewa na mamlaka ya maji safi na maji taka Tanga.

“Ombi langu kubwa ni kuwa hawa wafanyakazi wanaosoma mita hawana utaalamu wa kutosha, hivyo basi tunauomba uongozi wa mamlaka kuwapeleka shule. Inavyoonyesha hawajui, kwani kila mwezi kunakua na tofauti kubwa ya bili wanazozileta,” alisema Tarimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Joshua Mgeyekwa, amekiri kuwepo kwa tatizo na kuongeza kuwa watakutana na meneja wa huduma kwa wateja ili waweze kumaliza kero hiyo.

Inadaiwa kwamba wasomaji wengi wa mita za maji hawana elimu ya kutosha ya kazi zao, kitu kinachosababisha wateja wao kuwa na bili zenye tofauti kubwa ya uwiano kwa kila mwezi.

Na Bertha Mwambela, Tanga

Monday, December 6, 2010

SAFI MATONYA- UMETUWAKILISHA VYA KUTOSHA!

(Matonya na Davis ambaye pia ni mshindi wa Tusker Project Fame 4 wakiimba)

Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanga, Tanzania Matonya, jana alifanya show ya aina yake kunako mashindano ya Tusker Project Fame 4 wakati washiriki walipoimba na mastaa wa muziki ambao wanatambulika katika tasnia hiyo.

Matonya aliitwa baada ya mshiriki kutoka nchini Uganda anayejulikana kama Davis kuchagua kuimba na msanii huyo. Kwa pamoja waliimba nyimbo mbili za Matonya ambapo walifanya utambulisho wa Vaileti na muda kidogo wakaimba wimbo mwengine Anita. Hii ni heshima kubwa kwa msanii Matonya kuuwakilisha mkoa wa Tanga.

Hata hivyo katika hatua nyingine ya mashindano hayo Mtanzania pekee aliyeingia fainali hizo Peter Msechu aliweza kukamata nafasi ya pili huku Davis wa Uganda akiibuka mnyange.



Enjoy 'Anita' ya Matonya hapa.

Sunday, December 5, 2010

KUMBUKUMBU YA MZEE WETU KHALID ATHUMAN BYANAKU

It has been two years since you gone Dad but it still feels like yesterday. We miss you everyday, Thanks for the love you gave us B'coz We are everything we are today because of you.

We know are watching us in every single day, continue blessing so that We make you proud always. Your memories are eternally treasured forever. We will always love you dad, may your soul Rest in Peace.
Amin

Thursday, December 2, 2010

BOZI BOZIANA NDANI YA TANGA JUMAMOSI HII YA TAREHE 4

Mwanamuziki nguli wa miondoko ya soukous Mbenzu Ngamboni Boskill, maarufu kama Bozi Boziana anatarajiwa kufanya onyesho la aina yake jijini Tanga siku ya jumamosi ya tarehe 4 kunako uwanja wa Mkwakwani.

Imeelezwa kuwa katika onyesho hilo ambalo litakuwa la aina yake...kiingilio kitakukuwa ni shilingi elfu kumi tu.



Sio ya kukuosa mdau.

Wednesday, December 1, 2010

LEO NI SIKU YA UKIMWI DUNIANI!!

Siku ya Ukimwi Duniani inakumbukwa kila tarehe moja Desemba. Hii ni siku maalum ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa Ukimwi. Desemba moja ilichaguliwa kuwa ni siku ya Ukimwi kutokana na tarehe hiyo kuwa ndio siku ambayo kirusi cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981. Toka mwaka 1981 watu zaidi ya milioni 25 wameshafariki kutokana na Ukimwi.

Siku hii ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. Kuanzia hapo siku hii imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanaharakati.

Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS ililipa shirika lisilo la kiserikali la Kampeni ya Ukimwi Duniani (the World AIDS Campaign) wajibu wa kuratibu siku hii.

Kila mwaka siku hii hukumbukwa kwa ujumbe maalum. Ujumbe wa mwaka 2005 ni Zuia Ukimwi: Timiza Ahadi. Ujumbe huu utatumika hadi mwaka huu wa 2010. KAPIME UJUE AFYA YAKO EWE MDAU MTANZANIA, EWE MDAU WA 'VIJIMAMBO VYA TANGA'!

Tuesday, November 30, 2010

MJI WA TOLEDO, MAREKANI NDIO MJI DADA WA TANGA, TANZANIA!!

Toledo is the fourth most populous city in the U.S. state of Ohio and is the county seat of Lucas County. The municipality is located in northwest Ohio on the western end of Lake Erie, and borders the State of Michigan.

Tanga is both the name of the most northerly seaport city of Tanzania, and the surrounding Tanga Region. It is the Regional Headquarters of the region. The city of Tanga sits on the Indian Ocean, near the border with Kenya. Major exports from the port of Tanga include sisal, coffee, tea, and cotton.

Situated near the historic center of Toledo, Eurostars Toledo offers beautiful views of the city. It has an outdoor swimming pool, a chic restaurant, and spacious rooms with free Wi-Fi.

Tanga Beach Resort is not only the best luxury hotel in Tanga, it is also the best luxurious hotel for tourists and business travelers in Tanga, Tanzania. It started operations in the year 2009. The Hotel is located adjacent to the Indian Ocean in Tanga city which has a dynamic and historic past.