BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, December 23, 2009

ZAWADI WA X- MASS NA MWAKA MPYA KWA WADAU WA VIJIMAMBO VYA TANGA


Helo wadau wa VIJIMAMBO VYA TANGA najua mungu anawapenda na ndio maana hadi leo mpo kwani kuna waliotamani kuiona siku kama ya leo lakini kwa mapenzi yake mungu imeshindikana. Basi tuna kila sababu ya kumshukuru yeye kwani ndio muweza wa kila kitu hapa chini ya jua lake katatifu.
Tulipoanzisha VIJIMAMBO VYA TANGA tulikuwa pamoja na hadi sasa libeneke bado tunalisongesha. Basi niwatakie heri ya sikukuu ya X- Mass na Mwaka Mpya
Mohammed Hammie Rajab
Production Manager
ANKO MO BLOGSPOT
S.L.P 6184
TAMGA, TANZANIA
Phone: +255719000010

AY ATOA SOMO LA FUNGA MWAKA!!!


Nyota wa hip hop nchini AY amewapa somo kuwa mwaka 2010 utakuwa na maana kubwa katika muziki wa kizazi kipya kama wasanii wa hapa nchini wataamka na kusaka mafanikio nje ya mipaka.

"Wasanii wengi hapa nchini wanaonekana kuridhika kushindana wenyewe kwa wenyewe humu nchini," alisema AY

Haya si maendeleo, ni sawa na mtu anayekaa ndani mwake na kuona kuwa TV ya nchi 14 aliyonayo ni kubwa ya kutosha na makochi aliyonayo ni mazuri kabisa... anaona hivyo kwasababu hajatoka nje kuona changamoto tofauti.


Ndio maana nasema wasanii nchini tusiridhike kufanya shoo hapa Dar es salaam ama kusafiri kufanya shoo za Kigoma, na Arusha tu.
"Hii inatudumaza kimawazo kwasababu mawazo yetu mengi yanafanana. Tujaribu kutoka nje. Tujaribu kusonga mbele tusikubali kuishia shule ya msingi. Tuwe na mawazo ya kusoma sekondari hadi vyuo vikuu.


Tuesday, December 22, 2009

ZAHIR ZORRO AINGIA TENA STUDIO NA WANA BONGOFLAVA!!!

Baada ya kutoka na FID Q kwenye Ripoti za Mtaani.na kufunika saana Mzee Zahir Zorro, baba yake Banana anarudi tena na Mr. Blue & Baby Boy. Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Zahir Ally Zorro, katika kuonyesha ukomavu ameingia studio na nyota wa bongo fleva hao wanaotesa na sauti murua na kutengeneza kibao kikali kitakachokuwa kwenye miondoko ya Hip Hop.


Twende sasa!! Full kubanana na wanabongo flava

Sunday, December 20, 2009

SIO ISHU KUWA'DIS WALIOKUTOA- ASEMA AFANDE SELE

Mfalme wa Rhymes nchini, Seleman Msindi (Afande Sele) amewataka wasanii wanaochipukia na kukubalika wasijisahau na badala yeke warudishe fadhila kwa waliochangia mafanikio yao.

Afande aliyachana hayo huku kusisitiza kuwa ni upuuzi wa hali ya juu kwa msanii kuwaimba vibaya maprodyuza huku wakifahamu fika kwamba wahusika hawawezi kujibu. Kama hiyo haitoshi, Afande Sele amebainisha kwamba usanii huo unarudisha nyuma muziki wa kizai kipya.

"Tunatakiwa kuachana na ugomvi na kumkimbia shetani ili mambo yetu yawe mazuri," anasema afande. Anasema awali wasani walikuwa na tabia ya kuimba wapenzi wao kwa kuwataja majina lakini baada ya kukemea, tabia hiyo imekoma.


"Kinachotakiwa ni kuangalia matatizo yanayoigharimu nchi na kuyaibua katika tungo ili kusaidia maendeleo. "Najua wasanii wa Bongo hawataki kuambiwa ukweli ingawa ndivyo ilivyo, mfano ukimwambia msanii fulani anaimba kama fulani, hapo litatokea bifu wakati unatakiwa kukubali uhalisia.

(Huyu ni Afande Sele jamani)
Mfano mimi nafanana na Sugu katika uimbaji kwa kuwa ndipo nilipotokea siwezi kukataa,"alisema msanii huyo anayeuwakilisha vyema mkoa wake wa Morogoro na ambaye yupo katika hatua za mwisho kuachia track mpya itakayoitwa 'Kingdom', ambayo imegongwa studio za Bongo Records.





Friday, December 18, 2009

SAFARI YA KUTEMBELEA MBUGA YA SAADANI YAZIDI KUIVA!!

Gharama: 20,000/= chakula, vinywaji na kiingilio
Siku: Jumamosi, Tarehe 26/12/2009
Tiketi: Zinapatikana MWEKASU HOSTEL iliyopo karibu na Tanga Hotel.
Mawasiliano: 0713400730, 0786730400, 0718400203
Njoo uone ustaarabu wa mbuga ya Saadani, mbuga yenye vivutio mbalimbali vya kitalii

K-LYINN ATOA SINGO MPYA YA "I' M NOT A FLIRT"

Miss Tanzania 2000 Jacqueline Ntuyabaliwe, ametambulisha wimbo wake mpya wa “I’m Not a Flirt”. Mrembo wa Milenia Jacq, maarufu pia kwa jina lake la jukwaani la K-Lyinn, amesema jana kuwa wimbo huo ni kwa ajili ya albam yake mpya ambayo itatoka mwaka 2010.

“Hii ni single ya kwanza,” alisema muimbaji huyo wa Bongofleva. “Nimesharekodi baadhi ya nyimbo na huu ni mwanzo tu.”
Muimbaji huyo amesema wimbo huo umerekodiwa katika studio ya B.Hitz ya prodyuza bora wa mwaka jana wa tuzo za Kili Hermy B na unamfafanulia mpenzi wake kwamba yeye ni mtulivu katika mahusiano yao.

Unamaanisha kwamba niko kwenye mahusiano, mimi si mhangaikaji wa kimapenzi,” alisema mwanadada huyo. “Namweleza huyo mtu wangu kwamba asihisi kwamba mimi si mwaminifu katika mapenzi yetu,” alisema K-Lyinn bila ya kufafanua kama anajielezea yeye moja kwa moja.

K-Lyinn alisema wimbo huo ameuimba kwa lugha ya Kiingereza ingawa pia kiswahili kimo. Miongoni mwa mashairi katika wimbo huo yanasema: “Wanaume wananitolea macho lakini mimi ni wako, acha wivu.”

Akizungumzia sababu za kuamua kutumia lugha ya Kiingereza ambayo tungo zake hapa nchini zimekuwa zikikosa mapokezi mazuri kwa mashabiki. alisema “Tunawaimbia watu mbalimbali, hivyo tunapaswa kumgusa kila mmoja na pia tunalenga kujitanua kimataifa”

Muimbaji huyo anasema wakati fulani alipokuwa katika ziara zake za kimuziki nje ya Tanzania, alishaulizwa, “Huwezi kutuimbia kwa lugha tuijuayo?” “Ndio sababu nikaamua kutoka namna hii kivingine,” alisema muimbaji huyo aliyepotea kwa muda kwenye gemu ya muziki.

NIMEWAKUMBUKA MASUDI KIPANYA NA FINA MANGO

Najua utakuwa unakifahamu kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na redio Clouds Fm iliyopo jijini Dar es salaam. Kipindi hiko kwa sasa kinafanywa na Babra Hasan na Gerlad Hando...ila hapo awali kilikuwa kikifanywa na Fina Mango pamoja na Masoud Kipanya.

Dah washkaji walikuwa juu sana, mlitufanya tuwahi kuamka kwa ajili yenu. binafsi nilikuwa napenda sana kuwasikiliza wanavyoleta raha na kuibua hisia zilizokuwa zimejificha.

Walikuwa wanaleta masihara penye ukweli, lakini wakijaribu kudadavua yale ambayo yana mguso katika jamii ili wasivunje sheria za nchini.

Kipindi kilikuwa kimesimama kweli- Masoud tunajua kazi zake ila najiuliza Fina yupo wapi na anafanya nini kwa sasa..?

Pamoja na hayo tunawakumbuka sana, mlikuwa wa kwanza kukaribishwa bungeni na mkarushwa live na Mh. Spika wa Bunge Samweli Sitta.
We Miss U Guys!!!


Thursday, December 17, 2009

BLUE KURUDI TENA SHULE KWA AJILI YA KUJIFUNZA KIMOMBO


Mkali wa miondoko ya hip hop nchini, kutoka lebo ya micharazo, Harry Samir a.k.a Mr Blue, amekamilisha taratibu zote za kurudi darasani kwa ajili ya kujifunza umombo.


Habari kutoka pande za Ilala, yaliko maskani ya dogo huyo ‘tozi’ anayesumbua katika game la muziki wa Bongo fleva na kibao chake cha ‘Tupo pamoja’ zinasema kuwa, ameamua kuingia darasani kujifunza kiingereza na lugha nyingine kibao za kimataifa, ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuupeleka muziki wake kwenye ‘levo’ za kimataifa.

Mchizi huyo alikiri kuamua kurudi ‘skonga’ na akazidi kumwaga ‘data’ kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa muziki wake haufiki katika anga za kimataifa kutokana na kushindwa kuimba kwa lugha zinazoeleweka kimataifa. “Nguzo muhimu ya kufika huko ni kujaribu kuimba kwa lugha za kimataifa ambazo zinaeleweka nje ya mipaka ya Tanzania,” alitonya Blue

Tuesday, December 15, 2009

UNAWAJUA GREAT THINKERS WALIOTAMBA KUNAKO FASIHI ANDISHI NCHINI TANZANIA..??


(HAMMIE RAJAB)

Wadau wa blog na wale wapenda kusoma vitabu vya GREAT THINKERS ambao wameweka historia katika kutumia fasihi andishi nchini Tanzania. Kama kuna mtu anaweza kunisaidia kupata mtiririko wa vitabu hivi tafadhali awasiliane na mimi kwani ni HAZINA ILIYOJIFICHA.

Nimeona kuna haja ya kuwa na libraly ya vitabu hivi ili kutunza na kuenzi utamaduni wa mali zetu kupitia wahasisi hawa ambao hawatasahaulika/japokuwa wengine wapo mbele ya haki na wengine bado wangali hai.

Sitasahau kipindi kile upo darasani mwalimu anafundisha, mzee umeinamia kwa chini unaperuzi SANDA YA JAMBAZI- Maliki Mbowe alivyolitingisha jiji la Morogoro!!! Yeyote aliye na copy ya moja ya vitabu hivi
atakuwa amenisaidia sana...........

(FARAJI KATALAMBULA)

Ila mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Eddie Ganzel mahari pema peponi kwa alifanikiwa KUMSAKA HAYAWANI, moja kati ya watu ambao nilikuwa napenda sana vitabu vyao.
Pia Nilipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha mwandishi maarufu, Ben Mtobwa ama 'Joram Kiango'. Taifa lilipoteza kinara mwingine wa kutumia fasihi andishi kufichua masuala mazito yaliyoigubika jamii yetu.

Alitumia ipasavyo'mtutu wa kalamu' kufichua uzandiki na ufisadi katika jamii. Lakini upeo wa mwanadamu una kikomo.

(BEN MTOBWA)
Nawasihi tumpe mtunzi huyu 'ZAWADI YA USHINDI' kwa kusoma kwa undani vitabu vyake ili tutambue ni nini hasa amejaribu kutufunulia 'NYUMA YA MAPAZIA' ya jamii yetu iliyozingirwa na 'MALAIKA WA SHETANI' na
mafisadi wenye 'ROHO YA PAKA' wanaomsulubisha 'MHARIRI MSALABANI' na kudiriki kusema 'NAJISIKIA KUUA TENA' kupitia mikataba mibovu wanayoisaini 'DAR-ES-SALAAM USIKU' pasipo kumwambia mwekezaji uchwara 'PESA ZAKO ZINANUKA' na tena bila kuogopa 'SALAMU KUTOKA KUZIMU' au kilio chetu cha 'TUTARUDI NA ROHO ZETU?' Buriani Ben Mtobwa!

Nitayakumbuka sana haya majina: Hammie Rajab, Ben Mtobwa, Eristablus Elvis Musiba, Eddie Ganzel, Bawji, Sam Kitogo, Faraji Katalambula, Agolo Andulu, Kajubi Mukajanga, Beka Mfaume...na wengine wengi- hakika hawa ni GREAT THINKERS!!!

Hata hivyo vitabu ninavyovihitaji ni:
Kamlete akibisha mlipiue> Sanda ya Jambazi> Ama zake ama zangu> somo kaniponza> Najuta kuolewa> Tamu ya Haramu> Rest In Peace Dear Mother> Simu ya kifo> Lawalawa Tabora> Kikosi cha Kisasi> Kufa na Kupona> Hofu> Njama> Uchu> Mzizi wa Mbuyu> Malaika wa Shetani> Tutarudi na Roho zetu> Salam toka Kuzimu> Dar-es-Salaam Usiku> Najisikia Kuua Tena> Roho mkononi> Awe hai au amekufa namtaka> Nimekoma ukuwadi na shogayo hasidi> Kikomo> mikononi mwa nunda> Willy Gamba vyoote> Joram Kiango vyoote>

Tusaidiane kutunza hazina hii wadau




NGOMA MPYA (NAFASI) YA ALBINO FULANI KULETA MAPINDUZI


Jina lake kamili ni Babu Sinare. Hivi sasa makazi yake makuu ni pale Columbus,Ohio nchini Marekani. Ni msanii mpya wa muziki wa kizazi kipya.Jina lake la kisanii ni Albino Fulani.

He goes by the name of Albino Fulani who recently organized an outstanding benefit concert to raise funds to help kids with albinism by providing sun blocks to prevent skin cancer. He also participated in Baby Powder the movie and has just released a HIT new single NAFASI featuring Sugu and Belle 9 on chorus and Mwana FA on the 2nd verse.

The song was officially released on the Friday night show on East Africa Television (EATV) and it talks about things they will do if they were given a chance.

Monday, December 14, 2009

BIFU LA Q CHILLAH NA TID LATINGA POLISI (PART 2)

Bifu la wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohammed ‘TID’ na mwenzake Shabani Katwila ‘Q-Chiller’ lililoripotiwa hivi karibuni, limechukua sura mpya baada ya soo lao kutinga polisi.

Taarifa zimedai kuwa, bifu la wawili hao limefika polisi baada ya juzi kati Q-Chiller kuanza kumsaka mwenzake huku akiwa na silaha.

Akilonga, Meneja wa TID Khamisi Dakota alisema kuwa, Desemba 8 mwaka huu, akiwa maeneo ya Magomeni, Q- Chief alimvamia akiwa na wenzake wanne na kuanza ‘kumjazia inzi’ huku akimuuliza aliko TID.
Hata hivyo, kutokana na mazingira ya kutokuelewana kati ya wawili hao, inadaiwa Q-Chiller alianza kumsemea mbovu Dakota na mwishowe kuchomoa kisu na kutaka kumchoma.

Kufuatia hali hiyo, Dakota alikwenda moja kwa moja kuonana na TID ambapo walishauriana kulifikisha suala hilo polisi ambapo walikwenda kituo cha Magomeni na kufungua jalada la kesi lenye namba Mag/RB/22117/09 kutishia kuua kwa kisu.

NI KINGS AND QUEENS YA AMBWENE YESAYAH

Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava, kijana Ambwene Yesaya ametoka tena, safari hii kasimama wima na mrembo Jokate Mwegelo kunako Kings and Queens yakiwa ni mapinduzi mengine kunako sanaa yake, pia ni maandalizi ya kuufunga mwaka 2009 na kuufungua 2010.

Akilonga muda baada ya kudondoka Bongo akitokea pande za Kenya, alikokwenda kukamilisha mchongo wa pini hilo mchizi alisema kwamba ngoma ya Kings and Queens itatoka kwa staili ya video na kwamba kabla ya kusambaa kwenye runinga za TZ itaanza kuonekana MTV.

“Mbali na video hiyo ambayo nimeigonga Kenya kupitia Kampuni ya Ogopa pia kwa upande wa redio nimeachia kazi nyingine yenye jina la Bed and Breakfast ambayo imeifanyika ndani ya studio za B. Hitz Music Group chini ya Prodyuza Hermy B,” alisema A.Y.

Kitu kingine kipya alichosema Ambwene ni kwamba, kazi hiyo imefanyiwa mautundu zaidi (Mastering) katika studio za Ogopa Deejays. “Siku chache zijazo natarajia kwenda kupiga video yake na Kampuni ya Film Online iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini. Nawashukuru sana fans wangu, msichoke kunisapogti, sitawaangusha,” alisema.


Q CHILLAH NA TID WASHIKANA UCHAWI (PART 1)

The Big Names katika Bongo Flava nchini, Shabani Katwilla ‘Q-Chief’ na Khaleed Mohamed ‘Tid’ hivi karibuni wametoleana maneno ya kashfa kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa ni mchawi.

Ishu nzima iko hiviiii...juzi kati jijini Dsm, mtangazaji mmoja wa kike wa kituo kimoja cha televisheni aligonga mbili tatu hewani na msanii Q-Chief.

Wakiwa kwenye mahojiano ya laivu, Q-Chilah alisikika akisema kuwa tangu ameacha kufanya kazi na TID mambo yake yamekuwa hayaendi vizuri na kwamba tatizo hilo limekuwa ni la kudumu kwa upande wake.



Q-Chief aliendelea kusema siku moja akiwa katika mishemishe zake alikutana na mama mmoja (hakumtaja jina) aliyemwambia kuwa amelogwa na wasanii wenzake wawili akiwemo TID.


Q-Chief aliendelea kupigia msumari na kusisitiza kuwa, ni kweli amelogwa na wasanii hao na hakuna ubishi.


Kwa upande wa TID alisema kuwa, kauli ya Chilah imemdhalilisha sana hivyo ameamua kwenda kuripoti polisi na kwamba atahakikisha anamshughulikia kadiri ya uwezo wake.

Friday, December 11, 2009

SAFARI YA KUTEMBELEA MBUGA YA SAADANI


Gharama: 20,000/= chakula, vinywaji na kiingilio
Siku: Jumamosi, Tarehe 26/12/2009Tiketi: Zinapatikana MWEKASU HOSTEL iliyopo karibu na Tanga Hotel.
Mawasiliano: 0713400730, 0786730400, 0718400203
This is a unique National Park is located in the centre of the historical triangle of Bagamoyo, Pangani and Zanzibar. It is probably the only National Park in Africa where yuo can combine, a game drive or walking Safari and se Safari. Boat safaris can be arranged on River Wami "SAADANI- Where the sea, river and bush meets"
Saadani National Park Itinerary (Beach to Bush and River meet in a confusion of nature)Newest Saadan National Park is allocated 83 kms South of Pangani.
The word Saadan is created from mispronunciation of two Swahili Word Saa and ndani meaning a Watch and inside. Those two words were frequently spoken by one rich Asian Businessman who once lived in Saadan
Village during Arabic influence in the East Africa Coast.
The Businessman used these words to instruct his customers whowerecuriously and stubborn asking to be told time from a
differently device (wall clock) to get into the house to find time on their own.
This seemed new technology to the people in the village in telling time unlike to their original
African one they were used to. Laterthis man's home shop was nicknamed Saa ndani, mispronounced Saadani, Thus leading to the name Village.


Wednesday, December 9, 2009

KILA LA KHERI VICTORIA MARTINE- WATANGA WOTE WAPO PAMOJA NA WEWE

Aliyekuwa mnyange Miss Tanga 2007, Victoria Martine amekuwa ni mmoja kati ya warembo wawili watakaoiwakilisha Tanzania kunako mashindano ya urembo ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu, yanayotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 18.

Victoria Martine (20) na Juliet William (19) walichaguliwa kufuatia mchakato uliochukua takribani miezi mitatu huku ukiendeshwa na kamati maalum iliyochaguliwa na waandaaji wa Miss East Africa ambapo kamati hiyo ilikutana na warembo zaidi ya 150 kutoka sehemu mbalimbali Nchini ili kupata wawakilishi wawili wanaofaa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya urembo.



Victoria Martine, ni mrembo maarufu hapa Nchini ambae anajishughulisha na mambo ya mitindo, na pia amewahi kushinda tuzo ya reds fashion ambassador kwa mwaka 2007 Juliet William, yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha USIU cha jijini Nairobi, na pia ni mshindi wa tatu wa mashindano ya Miss Tanzania kwa mwaka huu.



Warembo wote wana viwango vinavyofaa kushiriki katika mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Africa.Mashindano ya Miss East Africa 2009ambayo yanasubiliwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa mambo ya urembo barani Afrika yatafanyika tarehe 18 mwezi huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, na yatawashirikisha warembo kutoka Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Ethiopia, Mauritius, Eritrea, na wenyeji Tanzania.



Mashindano hayo yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam, na kudhaminiwa na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, CMC Automobile, na AKO Catering Services.







JOH MAKINI AWATOLEA UVIVU WANAOTUMIA MASHAIRI YAKE KUTENGENEZA T-SHIRT

Mchizi kutoka A-Town (Arusha) Joh Makini amewamind masela ambao wanatumia mashairi ya nyimbo zake kutengenezea tshirt , kwa mfano ngoma ya 'STIM ZIMELIPIWA' tayari tshirt zimeshatoka nyingine za 'MWAMBA WA KASKAZINI'.

Makini anasema tshirt hizo hausiki nazo na anawaomba mashabiki zake kuto zinunuwa kwa sababu hazimuingizii chochote, na tayari anashughulikia ishu za kisheria kwa ajili ya hawa jamaa wanaopiga hayo magumashi.

NG'E 1982 YA MANGWEAR YAZIDI KUFANYA VIZURI MTAANI

Albert Magwea a.k.a Ngwea au Cow Bama inasemekana bado anaendelea kupiga bao kupitia mauzo ya albamu yake ya pili, N’ge 1982 ambayo imeshuka sokoni hivi karibuni ikiwa na ngoma zaidi ya 10.
Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo, albamu ya Ngwea ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya imeonekana kufanya vyema kitaani kutokana na ubora wake, zikiwemo kazi nyingi kali kama Nipe dili, Speed 120, Singida Dodoma, Mida Mibovu, CNN na nyingine.


Mabox yaiyosheheni abamu ya Ngwear

Ngwea ambaye alikuwa anagonga ‘buku’ pande za Bagamoyo Chuo cha Sanaa alisema kwamba nyimbo 15 kali zilizomo ndani ya albamu hiyo zimeifanya kuwa juu zaidi sokoni na kwamba amewataka mashabiki wake ambao bado hawajaifikia wajaribu kuisikiliza ili waone tofauti iliyopo na nyingine zilizotangulia mtaani.

“Kwa wale watakaohitaji kuinunua piga kupitia simu namba 0713 572323, 0754 999950,” alisema Cow Boy a.k.a Mwanachemba




Saturday, December 5, 2009

GET READY KWA SHANGWE ZA CHRISTMAS PARTY

INFINITY ENT'S pres,CHRISTMAS EVE Party 24th DECEMBER 09 at SPICE LOUNGE,3 savoy crecent, Theatre District,MILTON KEYNES.mk9 3pu,DJ HABIBU & DJ DOUBLE T will make it happen.
BONGO FLAVAS,R&B,RAGGA,OLD SKOOL. 10Pm till
Late,Admission:£10 B4 12:VIP TICKETS AVAILABLE AT THE DOOR- MZUXXX

TAZAMA COVER ALBUM YA MTU MZIMA SUGU

Hapa kwa mbele

Hapa kwa nyuma




C PWAA KUFANYA KWELI

Websites launch, Company launch, Clothes launch, Documentary, Xclusive performance,New song and Video Premier.Date: 8Th Dec 2009 From 9.00 pm for 15000/= ONLY!

TUNADHARAULIKA SANA NA BENDI ZETU- ASEMA TOP IN DAR

Kiongozi wa TOP Band, Khaleed Mohamed ‘T.I.D’ ameibuka na kuwashutumu vikali wadhamini wanaoshobokea kudhamini bendi za muziki zinazoundwa na wasanii wa kigeni hasa wakongo kuliko zile za wazawa.
TID alisema kuwa, imekuwa ni ngumu kwa mtu au kikundi cha watu fulani kuzisaidia bendi zilizoanzishwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama vile Top Band, Machozi Band ya Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ B-Band’ ya Banana Zorro na Bush Band ya Lucas Mkenda ‘Mr.Nice’ badala yake wanazikumbatia za wakuja.“Tunadharaulika sana, bendi zetu zinaonekana ni za wahuni.

Wadhamini wanaona bora wazisaidie bendi za wakongo kuliko zetu. Ukienda kuomba udhamini wanapiga chenga, lakini akienda mkongo anashobokewa kinoma,” alisema T.I.D.

FID Q KUONGOZA SHOW YA MTIKISIKO WA MASTAA IRINGA

Ngosha a.k.a Fareed Kubanda akiongozana na jeshi la zaidi ya watu nane wanatarajiwa kufanya show ya nguvu ndani ya mji wa Iringa kweny kile kinachoitwa Mtikisiko na mastaa.


Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika jumapili ya wiki hii ndani ya uwanja wa samora ambapo wataongozwa na Fid ni pamoja na Chegge, Matonya, Madee, Tundaman, Baby Madaha, Squeezer, Linex, Nay wa Mitego, Dully Sykes, Fell na wengine kibao.

“Mbali na kina Fid Q kufanya bonge la shoo siku hiyo, mabondia Rashid Matumla ‘Snake Boy’ na Chupaki wa Iringa,” watazichapa kuwania ubingwa usiyo rasmi,” alisema mratibu wa ishu hiyo, Eddo.





Saturday, November 28, 2009

DAZ NUNDAZ KURUDI TENA KWENYE RAMANI YA BONGO FLAVA!!

Kama unalikumbuka ni kundi lililowahi kutamba sana miaka ya 90 ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wawili Ferouz na Daz Baba ambao ndio walichangia kwa kiasi kikubwa kundi hilo kujipatia umaarufu wametangaza rasmi kumaliza tofauti zao.
Wakizungumza kwa pamoja, wasanii hao walidai kuwa kwa sasa wako tayari kufanya kazi pamoja na hata kulirejesha upya kundi lao la Daznundaz.

“Unajua tofauti zetu zilikuwa ndogo tu, ingawa vyombo vya habari vilichangia sana kuzikuza,hivi sasa tuko pamoja na mimi niko tayari kufanyakazi na mshkaji Daz Baba,” alieleza Ferouz, ambaye anaonekana kufulia kinoma kimuziki na kimaisha tofauti na alipokuwa na kundi la Daz nundaz.

“Mimi na msanii mwenzangu Larumba ambaye tulikuwa pamoja tulianzisha kundi letu la Tanzaniano , lakini hili halituzuii kukaa pamoja na Ferouz na washkaji wetu wengine ili kulirejesha kundi letu la Daznundaz. Ferouz ni mtu wangu na niko tayari kufanya naye kazi,” alisema Daz Mwalimu .
Kundi la Daznundaz lilisambaratika siku chache baada ya baadhi ya wasanii wake wakiongozwa na Ferouz kumtimua kundini msanii mwenzao Dazbaba kwa madai kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya ‘teja.’

Kundi hilo lilipata kutamba na nyimbo zake kali kama vile; Maji ya shingo, Kamanda, Barua, Jahaz la Daz na nyingine