BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, April 26, 2011

PUMZIKA KWA AMANI BABA YANGU HAMMIE RAJAB

(Hapa ndipo mwili wa baba yangu Hammie Rajab ulipohifadhiwa)

Tarehe 21/04/2011 nilifiwa na baba yangu mzazi Hammie Rajab, mazishi yake yalifanyika huko mkoani Morogoro katika makaburi ya Kola. Hakika lilikuwa pigo kubwa sana kwangu na familia yangu. Sitasahau kamwe kwani baba yangu alikuwa mtu makini sana hasa linapokuja swala la sanaa na utunzi wa vitabu. Aliandika vitabu vingi ikiwa ni pamoja na Sanda ya Jambazi, Kamlete Akibisha Mlipue, Somo Kaniponza, Nimekoma Ukuwadi, Rest In Peace Dear Mother, Ufunguo wa Bandia na vingine vingi. Pia aliwahi kuongoza filamu nyingi hapa nchini.

Nimeumia sana kumpoteza baba yangu japokuwa nimerithi kitu muhimu kutoka kwake, utunzi wa hadithi. Hakika maji yamefuata mkondo, kwani tayari hadi sasa nimeandika JINAMIZI ZA PASAKA, DISEMBA 26 pamoja na YALIYONIKUTA TANGA. Baba yangu huko ulipo.......nakuahidi kuendeleza kushika kalamu kama ambavyo ulivyoitumia na kujiwekea heshima kubwa. Ombi kwa serikali.....ijaribu kuwakumbuka na kuwaenzi waandishi na watunzi hapa nchini. Mungu akurehemu baba yangu Hammie Rajab.

(Natoa shukrani wa marafiki zangu wote waliokuwa bega kwa bega na mimi katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa baba yangu. Nawashukuru sana wadau wote wa VIJIMAMBO VYA TANGA pia pamoja na MARAFIKI WA TANNGA. Mmenifarji sana.)

No comments:

Post a Comment