BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, April 28, 2011

HABARI NJEMA KUTOKA TIGO KWA WAKAZI WA TANGA!


"Ukiwa TANGA kwa siku ya jumamosi ya tarehe 30/04/2011 karibu kwenye viwanja vya TANGAMANO ujionee tamasha la BUREE lililosheheni wasanii wakali kama 20 Percent, Juma Nature, Roma kutoka nyumbani TANGA pamoja na Afande Sele. Simu zitauzwa kwa BEI NAFUU na utapata nafasi ya kujisajili na TIGO PESA! Wote mnakaribishwa!

PILATO NA GAME YA BWANA MISOSI IPO HEWANI!!

Msanii kali wa Bongo Flava kutokea Tanga, Tanzania Bwana Misosi ameachia ngoma yake nyengine inayokwenda kwa jina la 'Pilato na game'....Misosi mwenyewe anasema!!

"Nyimbo yangu mpya inaitwa"pilato na game" nimefanyika pale Mj records chini ya producer Makochali na nimewashirikisha Nature na Fid Q na video imefanyika na Kalages picture na zote audio na video nimeziachia kwa pamoja."

Usikilize wimbo huo wa 'Pilato na game' hapo kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA. (Wimbo namba moja)


Wednesday, April 27, 2011

IFAHAMU COASTAL UNION YA TANGA

Coastal Union is a Tanzanian football club based in Tanga.

They play in the top level of Tanzanian professional football, the Tanzanian Premier League.

Their home games are played at Mkwakwani Stadium.


**********
Coastal Union Full name: Coastal Union
Ground: Mkwakwani Stadium
Tanga, Tanzania
(Capacity: 10,000)
League: Tanzanian Premier League

Achievements

* Tanzanian Premier League: 1

1988,

* Nyerere Cup: 2

1980, 1988

Performance in CAF competitions

CAF Cup Winners' Cup: 1 appearance

1981 - withdrew in First Round
1989 - First Round

Current squad

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

No.
Position Player
- Tanzania GK Ismail Suma
- Tanzania DF Leon Kimathi
- Tanzania DF Musola Thabit
- Tanzania DF Saadat Salum
- Tanzania DF William Basweku
- Tanzania MF Wiliam Juma

No.
Position Player
- Tanzania MF Dennis Taso
- Tanzania MF Ally Mkumbwa
- Tanzania MF Kudra Maguta
- Tanzania FW Uhuru Selemani
- Tanzania FW Hamada Kambangwa



Tuesday, April 26, 2011

PILI HASHIM NDIO MISS TANGA CITY CENTRAL 2011

Hatimae mnyange wa kitongoji cha Miss Tanga City Central amepatikana huku shindano hilo likiacha historia kubwa. Mwanadada Pili Hashim ndie aliyabahatika kuvaa taji hilo ambalo hapo kabla lilikuwa likishikiliwa na Anna Kiwambo mrembo wa kitongoji hicho kwa mwaka jana. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mishi Juma huku nafasi ya tatu ikienda kwa Salha Ibrahim. Kitongoji ca Miss Tanga City Central kiliandaliwa na kampuni ya Green Apple Entertainment kwa udhamini mkubwa wa Madam Hair Dressing Saloon, Mwanakodo, Sarah Issa, Arbab MB pamoja na Anko Mo Blogspot. Warembo wanne wamebahatika kuingia kunako kambi ya Miss Tanga 2011 ambapo kwa mwaka huu inaandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment na itafanyika tarehe 11/06/2011 pale Mkonge Hotel. Kabla ya hapo Miss Tanga ilikuwa ikiandaliwa na kampuni ya Five Brothers Entertainment.

Judith Kitogo ndie alikuwa mnyange wa Miss Talent 2011. Hata hivyo ndie aliyechukua nafasi ya nne na kubahatika pia kuindia kunako ambi ya Miss Tanga

Maximilan Luhanga ndie mkurugenzi wa kampuni ya New Face Entertainement yenye dhamana ya kuandaa Miss Tanga 2011. Hapa akimtangaza mnyange wa Miss Tanga City Central.

Pili Hashim na Mishi Juma ndio walibahatika kuingia fainali. Na hapa ilikuwa presha inapanda, presha inashuka mpaka alipotangazwa mshindi.

Top Five ya Miss Tanga City Central 2011....Pili Hashim (4), Rukia Shemdoe (1), Salha Ibrahim (3), Judith Kitogo (2) na Mishi Juma mwenye namba (5).....

Anaitwa Anna Kiwambo, ndie aliyekuwa anarudisha taji baada ya muda wake kumalizika. Anna Kiwambo pia ndie Miss Tanga 2010.

Mdhamini mkuu Jayesh Ranjiti maarufu kama J Pal akitoa burudani baada ya kuzungumza na watu waliohudhuria. Ilikuwa burudani tupu!!!

Kundi la Town Boys wakitoa burudani

Majaji wakijadili jambo na bibie Aisha ambaye ndie aliyeandaa shindano hilo kutoka kampuni ya Green Apple

Majaji wakiwa makini wakifuatilia warembo.

Warembo wa Miss Central wakipita na vazi la ufukweni.

Wakifungua show......

PASAKA NJEMA WADAU WOTE WA VIJIMAMBO VYA TANGA!


Blog ya VIJIMAMBO VYA TANGA inakutakia pasaka njema popote pale ulipo. Endelea kuitembelea kila siku kwa habari za Tanga na matukio yake.

PUMZIKA KWA AMANI BABA YANGU HAMMIE RAJAB

(Hapa ndipo mwili wa baba yangu Hammie Rajab ulipohifadhiwa)

Tarehe 21/04/2011 nilifiwa na baba yangu mzazi Hammie Rajab, mazishi yake yalifanyika huko mkoani Morogoro katika makaburi ya Kola. Hakika lilikuwa pigo kubwa sana kwangu na familia yangu. Sitasahau kamwe kwani baba yangu alikuwa mtu makini sana hasa linapokuja swala la sanaa na utunzi wa vitabu. Aliandika vitabu vingi ikiwa ni pamoja na Sanda ya Jambazi, Kamlete Akibisha Mlipue, Somo Kaniponza, Nimekoma Ukuwadi, Rest In Peace Dear Mother, Ufunguo wa Bandia na vingine vingi. Pia aliwahi kuongoza filamu nyingi hapa nchini.

Nimeumia sana kumpoteza baba yangu japokuwa nimerithi kitu muhimu kutoka kwake, utunzi wa hadithi. Hakika maji yamefuata mkondo, kwani tayari hadi sasa nimeandika JINAMIZI ZA PASAKA, DISEMBA 26 pamoja na YALIYONIKUTA TANGA. Baba yangu huko ulipo.......nakuahidi kuendeleza kushika kalamu kama ambavyo ulivyoitumia na kujiwekea heshima kubwa. Ombi kwa serikali.....ijaribu kuwakumbuka na kuwaenzi waandishi na watunzi hapa nchini. Mungu akurehemu baba yangu Hammie Rajab.

(Natoa shukrani wa marafiki zangu wote waliokuwa bega kwa bega na mimi katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa baba yangu. Nawashukuru sana wadau wote wa VIJIMAMBO VYA TANGA pia pamoja na MARAFIKI WA TANNGA. Mmenifarji sana.)

Tuesday, April 19, 2011

MISS TANGA CITY CENTRAL NI JUMATATU YA PASAKA!

Ukumbi: Railway Club

Siku: Jumatatu ya pasaka

Tarehe: 25/04/2011

Kiingilio: 5,000/= viti vya kaiwada
10,000 V.I.P


Kama unahitaji tiketi mapema piga namba hii 0715393996




Monday, April 18, 2011

MATONYA YUPO SHULE!

Watu walikuwa wakijiuliza Matonya yuko wapi mbona kimya, hatimaye imefahamika kuwa alikuwa kwenye tour huko Mombasa Kenya. Ila wakati yupi Nairobi alikuwa studio akitengeneza wimbo na msanii wa huko huko Nairobi anajulikana kwa jina la Nonini, mbali na Nairobi pia ameshatengeneza biti kwa producer Dunga na akirudi anaishughulikia na wimbo huo ameupa jina la "UTAKWENDA KULA ULIPOPELEKA MBOGA".

Pia Matonya ambaye anatokea Tanga amesema kwa sasa anapiga kitabu kule Kenya ila amesema ni mapema sana kusema anachokisomea mpaka akipata cheti ndio atasema alikuwa anasomea nini. Kwahiyo amewaomba mashabiki wake kwa sasa wawe wapole tu mnyamwezi wenu atakuwa kitaani muda si mrefu.

MBUNGE TANGA AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO!

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga kupitia chama cha wananchi (CUF) Amina Mohamed Mwidau (kushoto) ameahidi kuendeleza michezo katika mkoa huo na kuwataka vijana kuvunja makundi ya kushinda vijiweni na badala yake kuelekeza nguvu zao katika shughuli za kimaendeleo na michezo.

HONGERA JANUARY MAKAMBA!

Anko Mo Blogspot inakupa hongera mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga Mh. January Makamba kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC na katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Hii inaonyesha ni kiasi gani mkoa wa Tanga ulivyo na viongozi shupavu kama ambavyo mheshimiwa rais Jakaya Kikwete alivyomteua mbunge wa Tanga mjini Mh. Omary Nundu kuwa waziri wa uchukuzi. Tanga Ooyee!!

Friday, April 15, 2011

FILAMU YA FUKWE YAANIKA HISTORIA YA TANGA

BIASHARA ya utumwa katika Pwani ya Tanzania Bara , ilikuwa na faida kidogo. Biashara hiyo ililetwa na Waarabu ambao waliwashawishi wenyeji kwa zawadi ndogo na kujikuta wameingia katika kazi ya kukamata watumwa na kuwauza kwa Waarabu hao. Wananchi wa Bara na Pwani, walikuwa ni wenye nidhamu na heshima kulingana na mila na desturi za kila kabila.

Kama kawaida yao, ukarimu huo uliwagharimu wema bali mahasidi waliotaka rasilimali watu yaani watumwa. Moja ya mikoa ya Tanzania iliyoathiriwa na mfumo wa biashara ya utumwa ni Tanga. Hali hiyo ilitokana na kuingia kwa desturi na utamaduni, ambao baadhi ya vizazi vya koo zilizokuwa zinashirikiana na wafanyabiashara hao waliziiga.

Idadi kubwa ya wakazi wa sasa wa pwani ya mkoa wa Tanga, si wenyeji wa asili ya maeneo hayo, bali ni kizazi cha watumwa waliouzwa kutoka Tanzania Bara, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Zambia, Zimbabwe, Rwanda na Burundi, Msumbiji na Malawi. Historia inaeleza kuwa watumwa walipokamatwa walitembezwa maelfu ya kilometa, wakipelekwa katika vituo mbalimbali vya kukusanyia vilivyotapakaa pwani ya Tanzania Bara, kuanzia Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.

Katika mikoa hiyo minne, Tanga ndiyo uliongoza kwa kuwa na vituo vingi zaidi. Uchunguzi wa mwaka mmoja na nusu uliofanywa kwa ushirikiano wa serikali na Mradi wa Uandishi na Utengenezaji wa Filamu za Historia ya Taifa iliyoitwa Fukwe za Dhahabu, uliondeshwa kati ya Februari 2009 na Septemba 2010 mkoani Tanga, unaonesha kwamba, mkoa wote ulikuwa na zaidi ya vituo arobaini na mbili...............

Kusoma zaidi BONYEZA HAPA



Makala hii imeandikwa na Anna Makange, Tanga.

T.M.D KUNDI LA DANCE UTOKA TANGA!

Locatio: Tanga, Tanzania

About: T.M.D NI ORGANISATION AMBAYO INASHUGHULIKA NA MAMBO YA SANAA IN TANga tanzania

Personal Information: Wale wakazi wa tanga hili ni kundi madhubuti xana kwa upande wa dance. Ninafanya kazi kwa uzoefu wa hali ya juu kwa yeyote ambaye anataka burudani asisite kuwasiliana na sisi kwani utapata kile kitu utakacho................

Email: shabco2001@gmail.com

Phone: 0688699000; 0656511620

Wednesday, April 13, 2011

SUMA LEE, C PWAA BIFU LAANZA UPYA!



Wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Parklane kutoka Tanga City, namzngumzia Suma Lee pamoja na Cp a.k.a C Pwaa wameingia kwenye bifu tena kimtindo....Habari zaidi kutoka kwenye Blog ya Dj Fetty zimesema kuwa.....Siku za karibuni tulimskia cp wakati wa uzinduzi wa album yake akitangaza kuwa yeye na Suma lee wamerudi pamoja na kurudisha kundi kama Parklane lakini baada ya kupiga show ya uzinduzi na Cp kwenye uzinduzi wake, hivi karibuni Sumalee ametoa mpya baada ya kudai kuwa Cp hajamlipa pesa zake zote badala yake alimpatia nusu na kudai kuwa show haijafanya poa yaani haikumlipa

, "kwanza alidanganya kuwa parcklane itarudi lakini sio kweli, parklane irudi kwenye uzinduzi wake tu?, mwambieni kuwa hizo pesa alizonidhulumu kama ye anaona ni kidogo mi zinanitosha kwa kilo mbili za gomba" amesema Sumalee

20 PERCENT NDANI YA TANGA JUMAMOSI HII!!!!

Msanii nguli wa muziki wa Bongo Flava nchini aliyejinyakulia tuzo tano kwa mpigo hivi karibuni kunako tuzo za Kili, Abbas Hamisi maarufu kama 20 Percent anatarajia kufanya show ya aina yake jijini Tanga siku ya jumamosi ya tarehe 16/04/2011 kwenye klabu ya kisasa ya La Club Lacasa Chica.



Show hiyo iliyoandaliwa na Mb Entertainement kiingilio kitakuwa ni shilingi 5000/=....Tukutane hapo!!!

MASIKA YAANZA KULETA MAAFA TANGA

MVUA za masika zilizoanza kunyesha kwenye maeneo tofauti nchini kuanzia katikati ya Machi, 2011, zimeanza kusababisha madhara kwa baadhi ya wakazi wa wilaya za Mkoa wa Tanga.

Mpaka sasa mvua hizo zimesababisha vifo vya wakazi wanane ambao saba ni kutoka wilaya za Handeni na Kilindi na mmoja jijini Tanga na uharibifu wa mali kutokana na miti mikubwa mikongwe kuanguka.

Akithibitisha vifo hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Jaffar Mohamed alimtaja marehemu Hamisi Hassan (45) mkazi wa Kata ya Makorora jijini Tanga ambaye alikufa juzi baada ya kuangukiwa na mti mkongwe kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyokuwa ikinyesha hapa.

“Jumapili jioni majira ya saa 10 nilipata taarifa kwamba jirani na Soko la Uzunguni kuna mfanyabiashara wa kunoa visu (Hassan) ameangukiwa na mti mkubwa pamoja na magari kadhaa baada ya kusukumwa na upepo mkali wakati mvua ikiendelea kunyesha. Marehemu huyo alikuwa ameumia vibaya kichwani na alifariki muda mfupi akiwa Hospitali ya Bombo alikokuwa akipewa matibabu,” alisema Mohamed.

Akizungumzia matukio ya vifo vingine saba vilivyotokea wilayani Handeni na Kilindi, alisema vimetokana na watu hao kusombwa na maji ya mvua wakati walipokuwa wakijaribu kuvuka mito iliyokuwa imefurika maji.

Alisema chanzo cha vifo hivyo ni wanavijiji kuamua kuweka mazoea ya kupita kwenye njia au maeneo ambayo yana mikondo ya mito ya muda mfupi pasipo kuhofia nguvu na kina cha maji yaliyopo.

“Unajua wakati mwingine mvua hizi za masika zimekuwa zikinyesha mfululizo mpaka siku hivyo wakati mwingine unakuta mwanakijiji amezoea kupita njia fulani ambayo ina mkondo wa mto hivyo bila ya kupata uhakika wa kina cha maji katika eneo kama hilo unakuta mtu anaamua kuvuka mto au mkondo huo wa maji kwa mazoea tu na hatimaye maji humshinda nguvu na kuzama,” alisema.

Amewatahadharisha wananchi kuacha mazoea ya kupenda kuvuka kwenye maeneo yasiyo rasmi hasa yenye mito ya maji pamoja na kukaa chini ya miti mikongwe wakati mvua zinapoendelea kunyesha.

Aidha, amewataka wazazi kuhakikisha wanaongeza uangalizi na usalama kwa watoto wao wadogo hasa wanaoenda shule kwa kuhakikisha wanarudi nyumbani kwa muda unaostahili wanapomaliza masomo ya siku ili kudhibiti uwezekano wa kuzurura ovyo, hivyo kukumbwa na ajali zinazoweza kusababishwa na mvua


Na Anna Makange, Tanga

Tuesday, April 12, 2011

NI TWANGA PEPETA IJUMAA HII NDANI YA TANGA!

Dansa wa bendi ya Twanga Pepeta!



Kundi zima la Twanga Pepeta watakuwa jijini Tanga ijumaa hii ya tarehe 15 ndani ya ukumbi wa Splendid.

MISS COLLEGE 2011 TANGA NI MOTO!

Baadhi ya walimbwende wa kitongoji cha Miss College Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao yak ila siku yanyofanyika kwenye ukumbi wa Splendid jijini hapa. Mchakato wa kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 umeanza na tayari baadhi ya vitongoji vimeshaanza mazoezi huku kila kitongoji kikionyesha nia ya kutwaa taji hilo. Vitongoji vingine vilivyoanza mazoezi ni pamoja na Miss Chumbageni, Miss Handeni, Miss Lushoto pamoja na Miss Tanga City Central. Miss Tanga 2011 inaandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment

Mshiriki wa kitongoji cha Miss College 2011

Mshiriki wa kitongoji cha Miss College 2011

Mshiriki wa kitongoji cha Miss College 2011

Mshiriki wa kitongoji cha Miss College 2011

Mshiriki wa kitongoji cha Miss College 2011... (Kumradhi kwa kutotoa majina yao, endelea kufuatilia Blog kwani bado mchakato unaendelea)

Friday, April 8, 2011

NEMBO MPYA YA VODACOM

Ujio mpya wa Vodacom nchini Tanzania

AFRIKA FEST NDANI YA ASCHAFFENBURG NDANI YA UJERUMANI

Wakazi wa mji wa Aschaffenburg,nchini Ujerumani wanatarajia kufungua msimu wa siku za joto kwasherehe za AFRIKA FEST, mjini Aschaffenburg,huko nchini ujerumani aka Ujeuri man.Shamra shamra hizo za asiye na mwana abebe jiwe ,zinatarijiwa kuanza siku ya tarehe14 April hadi16 April 2011,ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya sanaa,mziki na utamaduni kwa ujumla.

Na bendera ya Tanzania piga ua inawakilishwa na Dj maarufu "Mfundo pita"ambaye mwaka jana tualitajwa na redio mabali mbali nchini ujerumani kuwa ni DJ "Mkali wa midundo" ya World beat.Mji wa Aschaffenburg,nchini Ujerumani mwaka huu 2011 ndio mji wa mwanzo kufungua dimba la sherehe za msimu wa joto nchini humo,sherehe hizo zinatarajiwa kuudhuriwa na maelfu ya
wa watu kutoka kila kona ya ujerumani, Mnakaribishwa wote..

kwa maelezo zaidi wasiliana simu +49(0)1733779720, +49(0)1733779720 au ndani ya ujerumani pia
01733779720


Wednesday, April 6, 2011

RAJAB NAE NI MSHIRIKI WA SHINDANO LA RUKA JUU KUTOKA KILINDI TANGA


Jina: Rajab Mnyamisi Mgongwe

Umri: Miaka 28

Biashara: Mzalishaji na msambazaji umeme

Namba ya ushiriki: 05





Ukifika kijiji cha Gombero wilayani Kilindi, Tanga, ukauliza kumuona Rajab, utaulizwa “yule wa umeme?” ingawa kuna Rajab wengi mitaa ile. Kijana huyu ni mzalishaji na msambazaji umeme pekee eneo hilo tangu 2008. Rajab pia ni mkulima na mfugaji na aliianza biashara yake hii ya kutoa huduma ya umeme kwa mtaji wa kilo kumi tu za mbegu ya maharage alizopanda shambani mwake.

Alipovuna Rajab alipata kilo 40 ambazo alipanda tena na kupata magunia manne ambayo baadhi alihifadhi kama akiba ya chakula na mengine mbegu kwa msimu uliofuata. Alipopanda tena akavuna magunia 10 na ndiyo aliyoyauza na kupata fedha za kwenda kununulia mashine ya kuzalisha umeme.

Rajab ni mshiriki wa shindano la kumsaka mjasilia mali linaloitwa RUKA JUU chini ya Femina HIP....BONYEZA HAPA upate kujua mengi kuhusu shindano hilo

NOEL NI MSHIRIKI WA SHINDANO LA RUKA JUU KUTOKA TANGA


Jina: Noel Joseph Mbelwa

Umri: Miaka 26

Biashara: Muuzaji wa Vinywaji Laini vya Jumla

Namba ya ushiriki: 01




Noel anatoa huduma ya kuuza vinywaji laini kwa bei ya jumla katika eneo la Saruji mkoani Tanga. Baada ya kumaliza elimu ya msingi Noel alijaribu kutafuta elimu zaidi ikashindikana, kutokana na hali ngumu akaamua kuingia kwenye soko la ajira, nayo ikawa taabu.

Hatimaye alipofika Dar es salaam 2006/7 rafiki yake mmoja alimuunganishia kibarua katika kampuni ya SBC, watengenezaji wa vinywaji vya Pepsi. Ndipo Noel akaanza kazi ya kupakia na kupakua soda. Baada ya muda Noel na wenzake walipunguzwa kazi, akaenda Tanga katika hekaheka za kutafuta ajira.

Noel ni mshiriki wa shindano la kumsaka mjasilia mali linaloitwa RUKA JUU chini ya Femina HIP....BONYEZA HAPA upate kujua mengi kuhusu shindano hilo


MFAHAMU SAUMU MSHIRIKI WA RUKA JUU KUTOKA TANGA


Jina: Saumu Pongwe Liku

Umri: Miaka 29

Biashara: Duka la Vipodozi

Namba ya ushiriki: 02


Saumu anapatikana mitaa ya Kwaminchi mjini Tanga. Hapo ndipo lilipo duka lake la vipodozi, na mwendo kidogo kutoka hapo lipo duka lake lingine anakouza mavazi ya vijana wa kike na wa kiume. Baada ya kumaliza kidato cha nne Saumu aliamua kutafuta ajira. Aliajiriwa mara mbili lakini katika ajira hizo hakujiona akipata maendeleo.

Akaanza kujiwekea akiba ili ikimridhisha ajiajiri mwenyewe. Ilipofika hiyo siku akaacha kazi, wakati huo akiwa mwajiri wa kituo kimoja cha kuuza mafuta alikokuwa amefanya kazi kwa miaka minne. Akaanzisha biashara ya kuuza nguo kwa kukopesha. Biashara hii haikuwa rahisi kwani alijikuta akigombana na wateja kutokana na usumbufu wakati wa kulipa.

Saumu ni mshiriki wa shindano la kumsaka mjasilia mali linaloitwa RUKA JUU chini ya Femina HIP....
BONYEZA HAPA upate kujua mengi kuhusu shindano hilo