BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, January 13, 2010

ANGERIS AJA KIVYENGINE! SASA KUTOKA NA VIDEO KALI

Unamkumbuka alikuwa kwenye lile shindano la kuibua vipaji maarufu kama Bongo Star Search miaka ya nyuma, akaja akatoka na singl zake mbili ambazo zilimuweka kwenye soko la Bongo Fleva, hapa namzungumzia mwanadada mwenye mvuto Angeris.

Angeris akiongea hivi karibuni amesema yakuwa kwasasa yuko kwenye mchakato wa mwisho mwisho kumalizia kurekodi video ya wimbo wake wa “My Boo” ambapo siku si nyingi atatoa video yake.


“Yeah ni kweli kama ulivyosikia niko kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kurekodi video yangu ambayo siku si nyingi itakuwa kwenye vituo vya Televisheni ili kila mtu apate kuona ubora wa nyimbo zangu” alisema Angeris.

Katika tukio lingine ambalo ndio itakuwa kwa mara ya kwanza ni kuwa Video hiyo inatengenezwa ndani ya studio za Fishcrab chini ya Producer maarufu Lamar,hii ni kuonyesha maendeleo makubwa katika sekta ya muziki kwani studio nyingi siku hizi zinafanya na Video Production







No comments:

Post a Comment