
Mwanadada wa siku nyingi kwenye game la muziki wa kibongo Rehema Chalamalia a.k.a Ray C ameibuka na kusema hata waje wasanii wangapi wa kike lakini anaamini hakuna kama yeye kamwe na hakuna atakayekuja kuyafikia mafanikio yake.
Ray C au kama anavyojulikana kwa jina lingine kiuno bila mfupa aliyasema hayo baada ya siku za karibuni kuibuka wasanii wengi wa kike na kila mmoja kujitamba kwamba yeye ni zaidi ya wengine wote.

Ray C akiongea kwa hasira alizidi kusema “Lakini mimi hakuna demu wa kunitisha hapa Bongo si kwenye muziki sehemu yoyote ile, mi muziki nimefanya kipindi kirefu sana na mpaka sasa hakuna anayeweza kujifananisha na mimi, hakuna ambaye ameweza kufikia kiwango changu bado nipo mbali sana ndio maana napata shoo nyingi hata nisipotoa kazi mpya, nyimbo zangu hazichuji ukisikiliza ‘Na Wewe Milele’ sasa hivi hapo ulipo lazima usisimke lakini ni ya miaka mingi.” alimaliza Ray C
No comments:
Post a Comment