
Adili aliyasema hayo wakati wa utambulisho wa Filamu yake Mpya inayokwenda kwa jina la Loleza ambayo kwa kupitia kampuni yake mwenyewe ndio wamefanya kazi nzima. “Ni filamu mpya iliyochezwa na wasanii maarufu kama vile Mansu-Li, Buff G, na wengine kibao, kupitia kampuni yake ya Chapakazi Filmz,” alisema Adili

“Angalia kuanzia kasha lake hadi upigaji picha kusema kweli ina ubora wa hali ya juu sana, tuna uhaba wa maeneo ya kupigia picha lakini tuliliangalia hilo na tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kupata maeneo mazuri kwa kazi hiyo” alisema.
“Nimetumia miaka mitatu ku-plan mambo haya, ndio maana watu wakaona kama niko kimya, lakini nipo miaka yote nikipanga mageuzi katika filamu na majibu ni haya.” alimaliza kusema
No comments:
Post a Comment