BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, January 19, 2010

"SIWEZI KUMNYOOSHEA MTU KIDOLE WAKILISHA"- SHAA

Aniatwa Shaa kifupi cha jina alilolitumia kipindi yuko na kundi zima la Wakilisha lililokuwa linaundwa na vijana watatu Witness Mwaijaga, Langa Kileo na yeye Mwenyewe Sarah.

Akiongea wakati akijibu swali la nini kilichopelekea kuvunjika kwa kundi la Wakilisha Sarah alisema ya kuwa hawezi kumnyooshea mtu kidole kuwa alihusika moja kwa moja kuvunjika kwa kundi hilo kwani hata yeye alihusika.

“Siwezi kumnyooshea mtu kidole kwasababu hata mimi nilihusika katika kuvunjika kwa kundi,” alisema Sha ambaye alikuwa wa kwanza kujitoa katika kundi hilo kabla memba waliosalia nao kila mmoja kushika njia yake.

Muimbaji huyo amesema utoto ulikuwa umetawala wakati huo na hivyo akajikuta akisikiliza maneno ya uzushi kutoka kwa watu na kujikuta akichukua uamuzi wa kujitoa kundini.

Baada ya Sara, ambaye alikuwa akiimba viitikio vya nyimbo za Wakilisha kujitoa kundini, memba waliosalia Witness na Langa wakalipunguza jina lao na kujiita Wakili na wakarekodi wimbo ulioitwa ‘No Chorus’, ambao kama jina lake lilivyo haukuwa na kiitikio.

Sara hakuona sababu ya kuacha historia yote ya Wakilisha ifutike katika sanaa yake baada ya kujitoa kundini, hivyo baadaye akaamua kuchukua jina lililotemwa na wenzake kutoka kwenye jina la Wakili - SHA.


“Hata hivyo, sikugombana na yeyote miongoni mwa memba wa kundi,” alisema Sha.“Ndio maana katika nyimbo zangu ninazoandaa sasa, nawashirikisha wote wawili ili kufuta hisia zozote mbaya zinazoweza kuwepo kufuatia kuvunjika kwa Wakilisha.”

Sha amesema anaendelea vyema katika maandalizi ya albam yake ya kwanza tangu aanze muziki lakini hataki kuizungumzia sana kwasababu iko katika hatua za mwanzo.“unajua mimi napenda vitu vilivyo kamili, hivi sipendi kuzungumzia vitu ambavyo havijakamilika.” alimalizia Shaa







No comments:

Post a Comment