BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Saturday, January 2, 2010

MAGOFU YA TONGONI- FAHARI YA UTALII MKOANI TANGA


Tongoni ni jina la kata ya Wilaya ya Tanga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania. Kwa
mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 4,042 waishio humo.

Inapatikana kilometa 17 kusini mwaka mkoa wa Tanga, ni maarufu kwa Magofu ya kale yanayopatikana kwenye kata hiyo- ambapo inaelezwa kuwa magofu hayo yalitokana na msikiti uliokuwapo tangu karne ya 15.

Kichanja kwa ajili ya kupumzika- Magofu ya Tongoni yapo karibu na bahari.

Historia inaeleza kata ya Tongoni ilikuwa inakaliwa na kabila la Wadebuli, ambao walitokea barani Asia eneo la Dabhol Magharibi na Pwani ya ya India.
Mandhari ya eneo la Tongoni, nyuma ya picha hii ndipo magofu yanapopatikana.
Vasco Da Gama, baharia kutokea nchini Ureno alipata pia kutembelea magofu ya
Tongoni mnamo April mwaka 1498, ambapo alipata kula machungwa ya asili na kudiriki kusema kuwa ni matamu zaidi ya yale yanayopatikana nchini kwake.
Hata hivyo mwaka unaofuata alitembelea tena magofu hayo ya Tongoni na kukaa hapo kwa siku 15.

Hili jiwe, linaonyesha nyayo za waumuni wa dini ya kiislamu waliukuwa wakisugulia miguu yao kabla ya kuingia msikitini kusali. Ni Jiwe la kihistoria linalopatikana Tongoni pia

Mzee akielezea historii ya Magofu ya Tongoni

Tongoni ni moja kivutio kukubwa cha utalii kinachopatikana hapa mkoani Tanga, Tanzania. Vivutio vyengine vinavyopatikana mkoani Tanga ni Mapango Ya Amboni, Amani Natural Reserve, Hot Spring (Chemchem Ya Maji Moto), Mkomazi National Park, Saadani National Park pamoja na Pangani.

No comments:

Post a Comment