BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Saturday, January 30, 2010

MAISHA PLUS SASA NI VITA!!

Wakiwa tayari wameshaingia kwenye kijiji cha Maisha Plus mshiriki Kauthur Mohamed ameonesha nia ya kweli kulipiza kisasi mara baada ya kusema wazi ya kuwa atahakikisha analipiza kwa wale wote waliomchaguwa kutoka wiki iliyopita ambapo aliponea tundu la sindano.

Kauthur ambaye kwa wiki mbili mfululizo aliingizwa katika kundi la washiriki wanaotakiwa kutoka na mara zote hizo kuokolewa na kura za wananchi.

Wiki iliyopita alipopewa muda wa kuwashukuru wananchi kwa kumuokoa alitumia muda huo kutanganza hali ya hatari kwa washiriki wenzake ambao alipata kuwatambua mara baada ya waandaji kuonyesha ni nani na nani amempigia kura ya kutoka mwenzake.

“Mi natangaza beef kabisa kila mmoja ajuwe, yani kama wewe ulinipigia kura ya kutoka nakuambia ukae tayari lazima na mimi nikunyooshe kidole tu kwani kitu gani” alisema mshiriki huyo ambaye anaonekana ni mbabe kwenye shindano hilo.

Kufwatia hali hiyo baadhi ya wananchi wamesema ya kuwa Maisha Plus ya mwaka huu inaelekea kuchangamka kutokana na uhalisia wanaouonyesha washiriki.

“Unajuwa toka mwanzo ni kama mashindano yalipoa hivi lakini lakini naona sasa washiriki wamekuwa wakali na kuelewa nini maana ya mashindano hayo” alisema Juma Ali mkazi wa Tegeta.No comments:

Post a Comment