BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, January 13, 2010

HIVI UNAJUA KAMA LOON AMEBADILI DINI NA KUWA MUISLAMU..!!

Loon kama anavyoonekana sasa akiongea na muandishi wa Aljazeera baada ya kutoka kuhij Macca. Mwanamuziki wa Hip Hop toka Marekani Loon ambaye alishawahi kufanya ziara nchini Tanzania ametangazwa kubadili dini na kuwa Muislamu. Loon ambaye kwa sasa anajulikana kama Amir Junaid Muhadith.

Loon alikuwa mmoja wa wana Bad Boys akiwa chini ya Lebo ya Bad Boy Record kundi linaloongozwa na Puff Daddy a.k.a P Diddy akiongea na Al-Jazeera Loon anasikika akisema "Bad Boy days are over.

Now I am what you call a Good Boy." Kwenye Video hii Loon anasikika akiongelea maisha yake toka Mwanamuziki wa rap hadi kwenye uislamu. Loon alifanya mahojiano haya alipokuwa njiani akitokea kwenye Hijja huko Saudi Arabia. Habari hii ni muda kidogo lakini si vibaya kushare na wadau wa VIJIMAMBO VY TANGA!!

Loon alishwahi pia kuja Tanzania (Bongo) na kufanya kazi na studio za Agies Record na kutoa wimbo ulioitwa LOON BONGO ambao alishirikiana na Ibra da Hustle wa Nako 2 Nako na Prodyuza Ambros wa Mandugu Digital

No comments:

Post a Comment