BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, January 26, 2010

NINI HATMA YA COASTAL KATIKA FAINALI ZA LIGI DARAJA LA KWANZA ..?

Kwanza napenda kuupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kuifikisha hapo ilipo kwa sasa kwani ni mahali pazuri sana hata wakazi wa mkoa huo wamerudisha imani na timu yao lakini hebu tujiulize Jukumu zima la kutafuta wadhamini wa kuisaidia timu hiyo ni la nani? Nafikiri jibu litakuwa ni letu sote, na kama jukumu ni letu sote sasa mbona wanatanga tumejisahau na kuiachia klabu yenyewe ndio itafute wadhamini peke yake?

Na wadhamini wenyewe wakati mwingine huonekana kusuasua wakati timu yetu ina ukata wa fedha huku ikikabiliwa na michuano ya nusu fainali za ligi daraja la kwanza ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao kwa hiyo tunaisaidiaje timu? Au ndio kusema Tanga kunani? Lakini hebu tuachane na mambo hayo ya Kiswahili ambayo hayana msingi wowote katika kuinua kiwango cha soka letu katika mkoa wa Tanga.

Mabingwa hao wa soka wa ligi kuu ya Tanzania Bara wa mwaka 1988 kwa sasa wanaelezewa kuwa ndio wanaoshikilia hatma ya soka ya Mkoa huu ambao ulikuwa unatisha miaka ya nyuma katika tasnia ya kandanda la hapa nyumbani na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Kama nilivyokwambia hii timu kubwa na yenye heshima hapa nchini, kwa hiyo ina wapenzi na wanachama katika mikoa mingi ikiwemo Dar es Salaam kwa hiyo labda nitoe wito kuwa wajitokeze na kuisaidia timu katika kipindi hiki ambapo iko katika hatua hii muhimu” anasema Salim Mazrui ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Coastal.

1 comment:

  1. Greetings from Argentina!!!
    Aro Geraldes
    www.arogeraldes.com

    ReplyDelete