BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, January 26, 2010

"NILIROGWA" - H BABA

Mmoja wa wanamuziki wanaofanya mtindo wa TAKEU style Hamis Ramadhan “H Baba” ameibuka na kuzusha madai ambayo ni ya kushangaza. Akiongea hivi karibuni, msanii huyo amedai kurogwa na mmoja wa wasanii wenzake ndio maana mambo yake mengi yalikwenda kombo siku za karibuni.

“Unajuwa mtu ataniona mimi kama naongopa lakini ukweli ni kuwa nilichezewa ila nilikuwa sijui nimekuja kungundua baada ya kupita pita kwenye tiba, nilianza kujihisi hivyo mara baada ya kugombana na watu wengi sana nikiwa sijielewi” alisema H Baba ambaye kwasasa anakiri kupona matatizo hayo mara baada ya kupata tiba toka kwa wataalamu wa miti shamba.

Alizidi kusema “ Unajuwa ni ukweli kabisa waswahili hawakukosea walivyosema kikulacho kinguoni mwako, kwani yote hayo yalikuwa yakifanywa na mtu wa karibu kabisa tena rafiki yangu mkubwa” alisema H Baba kwa uchungu.

Alimaliza kwa kusema “Matatizo mengi yalitokana na Irene, unajua watu wengi hawakupenda niwe na Irene, kwahiyo ili kunikomoa ikabidi waniroge, mimi na Irene tukawa hatuelewani, tunagombana mpaka tukaachana,” alisema H.

Hata hivyo H Baba alikataa kumuweka wazi mchawi wake huyo.No comments:

Post a Comment