BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, June 22, 2010

AJALI YA MUEMBE KIJIJI CHA 21 JIJINI TANGA!!!

Mti wa muembe ukipakiwa kwenye fuso ukiwa umekatwa vipande baada ya kuanguka na kuziba barabara kwenye eneo la kijiji cha 21 jijini Tanga.

Watu ambao walipewa tenda ya kukata mti huo na halmashauri ya jiji la Tanga wakiusambaratisha mti huo ambao unasemekana ulianguka kutokana na kuzeeka! lol

Hakuna mtu yoyote aliyeumia...ila baadhi ya watu niliozungumza nao walisema kuwa miti ya miembe katika barabara hiyo inaonekana kuzeeka sana, hivyo wanaomba hamlashauri ya jiji la Tanga kuikata ili kuepuka ajali.

Baadhi ya nyaya za umeme zikiwa chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya mti huo.

Ilibidi magari na baiskeli kupita pembezoni mwa barabara hadi zoezi la kukata mti huo vipande na kupakiza garini ulipokamilika.

No comments:

Post a Comment