BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, June 30, 2010

MKOLONI ATOA KIONJO CHA UCHAGUZI MKUU 2010

Mkali wa Mashairi aliyeng’ara na Kundi la Wagosi wa Kaya kutokea mkoani Tnaga, Fred Maliki a.k.a ‘Mkoloni’ amegonga topic ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, kwa kutoa kionjo cha wimbo wake mpya ambao unaelezea umuhimu wa viongozi bora.

Mkoloni maarufu kama 'Kinega' kwa sasa, aligonga ‘akapela’ ya verse moja mwishoni mwa wiki mbele ya waandishi wa habari, Makao Makuu ya CHADEMA, mara baada ya kukabidhiwa kadi na katiba ya chama hicho ambacho alijiunga nacho rasmi.Katika ngoma hiyo, Mkoloni aliwafyatua baadhi ya viongozi ambao wanaendelea kutumbua badala ya kuwasaidia wananchi wao.

Mkoloni alikabidhiwa kadi ya CHADEMA pamoja na mastaa wenzake wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Gerald Mwanjoka ‘G Solo’.

No comments:

Post a Comment