BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Sunday, June 6, 2010

AZIZA KHALIFA NDIO MISS PANGANI 2010!!

Mnyange wa Miss Pangani 2010 Aziza Khalifa akiwa katika uso wa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa wilaya hiyo. Mshindi wa pili alikuwa Asha Athumani huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Stella William. Wilaya ya Pangani imeweka historia baada ya kutoa Miss wa kwanza kwa mwaka huu wa 2010. Washindi wote watatu wameingia moja kwa moja kwenye mchakato wa kumsaka Miss Tanga ambapo kilele chake ni June 19 pale Tanga Beach Resort. Shukrani kwa Pangani Coast Cultural Tourism Programme, Voda Com Tanzania, Mwekasu Hostel, Breeze Fm, na Sofia Production. Miss Pangani 2010 iliandaliwa na Anko Mo Blogspot

Aziza akiwa na mama yake mdogo.

Nickson, Mimi (Anko Mo) wa kati kati hapo- picha moja na warembo.
.Mimi nikiwa na warembo, pamoja na mwalimu.

Fady Dady akiwa na warembo.

Lunza akiwa na warembo.

Hongera.

Amina Sadiki ambaye alikuwa mwalimu wa warembo, akimvisha taji Miss Pangani 2010 Aziza Khalifa

Furaha tupu!!

Ilikuwa ngumu kujizuia. Watu wakija kutoa pongezi kwa mnyange wa Miss Pangani 2010

Hatimae....!!

Warembo wawili ndio waliobakia baada ya kutajwa tano bora. Aziza Khalifa na Asha Athumani.

Presha ilikuwa inapanda na kushuka, hii mikono ilikuwa ikitetemeka.

Nickson Lutenda kutoka Uzikwasa ambaye alikuwa mmoja wa majaji wa Miss Pangani akifuatilia kwa makini mchakato mzima.

Mwajuma Ally akivishwa taji na Lilian Mdachi.

Mwajuma Ally ndio alinyakua taji la Miss Talent 2010.

Fady dady, aliwapagawisha ipasavyo wakazi wa Pangani.

Full shangwe mazee! Dj Banja, Fady Dady, Untouchable na mshkaji.

Mkali wa Hip Hop kutokea Tanga City, anaitwa Untouchable alipiga bonge la show. Sikiliza wimbo wa msanii huyu hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Wimbo unaitwa 'Binadamu'

Palikuwa hapatoshi.

Mshereheshaji a.k.a swahiba wangu, Ally Mohammed maarufu kama Bra A akiongoza show nzima ya Miss Pangani 2010.

Majaji, wa kwanza Nickson Lutenda kutokea, wa pili Nassoro Makau ambaye ndie alikuwa chifu jaji. Na wengine kutokea 5 Brothers Entertainment ambayo inandaa Miss Tanga.

Cartoonist maarufu nchini Tanzania Marko Tibasima alikuwepo pia.

Mr Robert ambaye ni muakilishi wa Vodacom akifuatilia mchakato kwa makini.

Vijana wa Town Boys wakifanya mambo yao jukwaani.

Town Boys wakicheza ngoma ya asili.

Mtangazaji wa Mwambao Fm Leyla Totii a.k.a Mama Lao akitoa maneno machache jukwaani. Blandina Lukindo, Dj Bad Fuvu wote walikuwepo.

Watu wakifurahia Miss Pafurahia Miss Pangani 2010

Town Boys wakali wa Kiduku jijini Tanga wakiwa katika Pozz. Walifanya show za ukweli!!

Boka White a.k.a Dj Banja wa Pangani Fm aki'show love kwa wadau

Aliyevaa fulana nyeusi hapo mbele anaitwa George Mbara wa Breeze Fm. Wadau wengi walijitokeza kushuhudia Miss Pangani 2010

Mapaparazi walifanya kazi yao kwa uhakika!

No comments:

Post a Comment