BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, June 9, 2010

BIFU LA NATURE, RICH ONE HADHARANI

Siku chache baada ya kuenguliwa na swahiba wake 'Juma Nature' ndani ya kundi TMK Wanaume Halisi, Richard Shauri ‘Rich One’, amepanga kuanika kilichotokea hadi yeye na wasanii wengine kuenguliwa kundini na muasisi wa kundi hilo, Juma Kassim ‘Sir Nature’.

Akinukuliwa jana Rich alisema...."Mengi yamesemwa tangu mimi na wenzangu tulipoenguliwa kundini lakini nadhani kuwa sasa ni muda muafaka wa kuweka mambo bayana".

“Kaka tumepanga kukutana na waandishi wa habari kati ya Jumatano na Alhamisi wiki hii, ili kueleza kilichotokea TMK Wanaume Halisi, hata kudaiwa kuwa sisi tumetimuliwa,” alisema Rich One.

Tangu kuanzishwa kwa kundi hilo lililotokana na nyota hao kujitoa TMK Wanaume Family, hii itakuwa mara ya kwanza kwa wasanii kutimuana ingawa awali msanii Haruna Kahena ‘Inspekta Haroun’ alitangaza kujitoa mwenyewe na kufanya kazi zake binafsi.


No comments:

Post a Comment