BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, June 24, 2010

MWENGE ULIPOTEMBELEA SHIRIKA LA UZIKWASA PANGANI!

Meneja wa Pangani Fm Radio Ismail Mwishashi, akisomna risala kwa kiongozi wa mwenge kitaifa na mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zippora Pangani wakati mwenge ulipotembelea kituo hicho cha redio kinachotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni ambacho kipo chini ya shirika lisilo la kiserikali UZIKWASA (Uzima Kwa Sanaa)

Mwenge ukiwa chini ya ulinzi mkali, punde tu baada ya kuwasili UZIKWASA.

Mwenge!

Mwenge ukiwasili.

Ismail Mwishashi, ambaye ni meneja wa Pangani Fm akitazama kwa makini ujio wa mwenge.

Mimi (Anko Mo), Mr Urasa na dada Rukia wote wa UZIKWASA...tukisubiria mwenge.

Ilikuwa shamrashamra..kaka yangu Joseph hapo na dada Mariam wakiserebuka na mwenge.

Mhasibu wa shirika la UZIKWASA, Mr Tobias akiwa na Dr. Vera ambaye ni Mkurugenzi wa shirika hilo. Kwa nyuso za furaha wakisubiria ujio wa mwenge.

Afisa utamaduni wa wilaya ya Pangani Mr Semnangwa akisema jambo wakati mwenge ukiwasili.

Dr. Vera akiwa na Mr. Urasa.....Urasa ni Meneja wa shirika la UZIKWASA.

Vijana wa mwenge wakitoa burudani.

Mzee mzima Nickson Lutenda kutokea UZIKWASA, akifanya mambo. Kaka hapo alikuwa msema chochote.

Kikundi cha sanaa cha Kumekucha kutokea Madanga kikitoa birudani ya ngoma za asili.

Vijana wa mwenge wakiwasili.

Hiki ndicho kituo cha redio mpya ya Pangani Fm ambacho kinatarajiwa kufunguliwa wilayani Pangani mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment