BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, January 30, 2010

MAISHA PLUS SASA NI VITA!!

Wakiwa tayari wameshaingia kwenye kijiji cha Maisha Plus mshiriki Kauthur Mohamed ameonesha nia ya kweli kulipiza kisasi mara baada ya kusema wazi ya kuwa atahakikisha analipiza kwa wale wote waliomchaguwa kutoka wiki iliyopita ambapo aliponea tundu la sindano.

Kauthur ambaye kwa wiki mbili mfululizo aliingizwa katika kundi la washiriki wanaotakiwa kutoka na mara zote hizo kuokolewa na kura za wananchi.

Wiki iliyopita alipopewa muda wa kuwashukuru wananchi kwa kumuokoa alitumia muda huo kutanganza hali ya hatari kwa washiriki wenzake ambao alipata kuwatambua mara baada ya waandaji kuonyesha ni nani na nani amempigia kura ya kutoka mwenzake.

“Mi natangaza beef kabisa kila mmoja ajuwe, yani kama wewe ulinipigia kura ya kutoka nakuambia ukae tayari lazima na mimi nikunyooshe kidole tu kwani kitu gani” alisema mshiriki huyo ambaye anaonekana ni mbabe kwenye shindano hilo.

Kufwatia hali hiyo baadhi ya wananchi wamesema ya kuwa Maisha Plus ya mwaka huu inaelekea kuchangamka kutokana na uhalisia wanaouonyesha washiriki.

“Unajuwa toka mwanzo ni kama mashindano yalipoa hivi lakini lakini naona sasa washiriki wamekuwa wakali na kuelewa nini maana ya mashindano hayo” alisema Juma Ali mkazi wa Tegeta.







Friday, January 29, 2010

KAA TAYARI KWA SAUTI ZA BUSARA 2010

Wasanii watakaotoa burudani ni Thandiswa(Afrika Kusini), Nyota ndogo na Makadem (Kenya), Ba Cissoko (Guinea), Malick Pathe Sow (Senegal), Massar Egbari (Egypt), Banana Zorro, Fresh Jumbe, Chidi Benz (Tanzania) na wengi wengineo.

DAZ BABA KWISHAAAA!! ATUMIKISHWA HOVYO

Ni habari ya kusikitisha sana kwa msanii aliyewahi kuwa mkubwa kama Daz Baba kusikia habari kama hii.

Kutoka chanzo kimoja chini ya kapeti inasemakana Daz Baba ni kama Houseboy wa P Funk Majani pale studio za Bongo Record, kwani kila kitu hata sigara dukani jamaa hutumwa.

“E bwana utamuhurumia sana Daz, siku nzima anashinda pale studio kwa Majani na kila kitu anatumwa yeye hata kusafisha studio pale anasafisha yeye, yani Daz anasikitisha sana, dukani yeye, kuleta hata maji ya kunywa ni yeye” kilisema chanzo hicho

Jamaa alizidi kuongeza “yani anaweza kupita mara kumi hapa anaenda na kurudi dukani kama kitololi vile.” alimaliza

Daz Baba ni mmoja wa wanamuziki wa lile kundi lililotamba sana miaka ya nyuma Daz Nundaz ambalo alikuwepo yeye, Ferouz, Sajo, La Rhumba na wengine.

VIJIMAMBO VYA TANGA ilijaribu kwa kila hali na mali kumtafuta Daz Baba athibitishe hilo lakini simu yake ilikuwa haipatikani.







R.KELLY KUPIGA SHOW UGANDA LEO!

Mashabiki wa muziki,hususani wa R&B waliopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na hususani jijini Kampala nchini Uganda, leo watashuhudia onyesho ambalo hawajashuhudia ndani ya miaka kadhaa na huenda wasishuhudie katika miaka kadhaa ijayo. Hiyo ni ahadi,sio kutoka kwangu bali kutoka kwa mwanamuziki Robert Sylvester Kelly maarufu kama R.Kelly (pichani) kutoka nchini Marekani anayetarajiwa kufanya onyesho la aina yake leo jijini Kampala katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval.

Onyesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Zain,limepewa jina la “I Believe”. Hivi karibuni iliarifiwa kwamba kampuni ya Zain imetumbukiza zaidi ya $2.5 kwa ajili ya onyesho hilo kwani inasemekana kwamba kwa R.Kelly kukubali kufanya show yoyote nje ya Amerika Kaskazini basi $600,000 lazima ziwe mezani.

Viingilio katika onyesho hilo ambalo tiketi zake zilishakwisha(sold out) wiki mbili zilizopita, vimepangwa kuwa Ushs 30,000(Silver) Ushs 125,000(Gold) na Ushs 250,000(Platinum). Hii ni mara ya kwanza kwa R.Kelly kufanya concert katika ukanda wa Afrika Mashariki. Na barani Afrika kwa ujumla mahali pengine ambapo amewahi kufanya onyesho ni Afrika Kusini tu.

R.Kelly ameahidi kuimba nyimbo zake zote ambazo amewahi kutamba nazo kama vile Bump n’Grind, I Believe I Can Fly,Gotham City,Ignition(Remix),The World’s Greatest,If I could turn back the hands of time, na nyinginezo tele bila kusahau hip-hopera yake ya Trapped In A Closet.


Zaidi tembelea BONGO CELEBRITY






Thursday, January 28, 2010

'ZINDUKA' WIMBO MPYA WA KAMPENI DHIDI YA MALARIA

Kwa mara ya kwanza wasanii wa Bongo Fleva wamejumuika pamoja na kutunga wimbo kuhamasisha juu ya kujikinga na gonjwa sugu la Malaria.

Ni mkusanyiko wa kwanza ambao haujawahi kutokea katika historia ya muziki wa kizazi kipya kuweza kuwakutanisha wanamuziki kumi tano (15) wa muziki huo wa Bongo Fleva wakiwa wamechanganyikana na wakongwe wengine kwenye muziki huo kama vile Bi Kidude.

“Jina la wimbo unaitwa Zinduka na ni maalumu kwa ajili ya Kampeni za Malaria ambazo zinatarajiwa kufunguliwa na Mheshimiwa Rais mwezi ujao, wimbo wenyewe unawapa tahadhari wananchi kustuka na kuchukuwa kinga zaidi ya gonjwa hilo baya ambalo linaongoza kwa kuua Afrika” alisema mmoja wa wanamuziki aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo.

Baadhi ya wasanii waliosimama kwenye songi hilo ni Marlaw, Mwasity, Bi Kidude, Madee, Grace Matata, Ditto, Prof Jay na wengine wengi.




"CHID BENZ NI MKALI WA RHYMES"- AFANDE

Selemani Msindi a.k.a Afande Sele toka kundi la Watu Pori pande za Motown au Morogoro ameibuka tena lakini safari hii akiongelea anayeamini kuwa ni mtu pekee kwasasa kumvua taji lake la Mfalme wa Ryhmes.

Akichonga hivi karibuni Afande amesema ya kuwa anaamini kabisa kama kuna msanii wa Bongo fleva anayeweza kumvua taji lake basi ni Chid Benz toka kundi la LA Familia pande zile za Ilala

“Chid ni mkali wa mashairi, ana ryhmes, pia hata kuliburudisha jukwaa anaweza, mimi kwangu Chid ndio yupo juu kwasasa aisee, naweza kusema ndiye pekee anayeweza kuchukuwa taji la Mfalme wa Rhymes kwasasa.” alisema Afande Sele.

Afande Sele ndiye anayeshikilia taji hilo baada ya kufanyika mara moja tu miaka ya nyuma na kukutwa na misukosuko mingi.





Tuesday, January 26, 2010

"NILIROGWA" - H BABA

Mmoja wa wanamuziki wanaofanya mtindo wa TAKEU style Hamis Ramadhan “H Baba” ameibuka na kuzusha madai ambayo ni ya kushangaza. Akiongea hivi karibuni, msanii huyo amedai kurogwa na mmoja wa wasanii wenzake ndio maana mambo yake mengi yalikwenda kombo siku za karibuni.

“Unajuwa mtu ataniona mimi kama naongopa lakini ukweli ni kuwa nilichezewa ila nilikuwa sijui nimekuja kungundua baada ya kupita pita kwenye tiba, nilianza kujihisi hivyo mara baada ya kugombana na watu wengi sana nikiwa sijielewi” alisema H Baba ambaye kwasasa anakiri kupona matatizo hayo mara baada ya kupata tiba toka kwa wataalamu wa miti shamba.

Alizidi kusema “ Unajuwa ni ukweli kabisa waswahili hawakukosea walivyosema kikulacho kinguoni mwako, kwani yote hayo yalikuwa yakifanywa na mtu wa karibu kabisa tena rafiki yangu mkubwa” alisema H Baba kwa uchungu.

Alimaliza kwa kusema “Matatizo mengi yalitokana na Irene, unajua watu wengi hawakupenda niwe na Irene, kwahiyo ili kunikomoa ikabidi waniroge, mimi na Irene tukawa hatuelewani, tunagombana mpaka tukaachana,” alisema H.

Hata hivyo H Baba alikataa kumuweka wazi mchawi wake huyo.







NINI HATMA YA COASTAL KATIKA FAINALI ZA LIGI DARAJA LA KWANZA ..?

Kwanza napenda kuupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kuifikisha hapo ilipo kwa sasa kwani ni mahali pazuri sana hata wakazi wa mkoa huo wamerudisha imani na timu yao lakini hebu tujiulize Jukumu zima la kutafuta wadhamini wa kuisaidia timu hiyo ni la nani? Nafikiri jibu litakuwa ni letu sote, na kama jukumu ni letu sote sasa mbona wanatanga tumejisahau na kuiachia klabu yenyewe ndio itafute wadhamini peke yake?

Na wadhamini wenyewe wakati mwingine huonekana kusuasua wakati timu yetu ina ukata wa fedha huku ikikabiliwa na michuano ya nusu fainali za ligi daraja la kwanza ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao kwa hiyo tunaisaidiaje timu? Au ndio kusema Tanga kunani? Lakini hebu tuachane na mambo hayo ya Kiswahili ambayo hayana msingi wowote katika kuinua kiwango cha soka letu katika mkoa wa Tanga.

Mabingwa hao wa soka wa ligi kuu ya Tanzania Bara wa mwaka 1988 kwa sasa wanaelezewa kuwa ndio wanaoshikilia hatma ya soka ya Mkoa huu ambao ulikuwa unatisha miaka ya nyuma katika tasnia ya kandanda la hapa nyumbani na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Kama nilivyokwambia hii timu kubwa na yenye heshima hapa nchini, kwa hiyo ina wapenzi na wanachama katika mikoa mingi ikiwemo Dar es Salaam kwa hiyo labda nitoe wito kuwa wajitokeze na kuisaidia timu katika kipindi hiki ambapo iko katika hatua hii muhimu” anasema Salim Mazrui ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Coastal.

Monday, January 25, 2010

LILIAN MDUDA AULA M-NET FACE OF AFRICA!

Hatimaye Tanzania jana ilipata mwakilishi wake katika fainali za mashindano ya Kisura wa Afrika yanayotarajiwa kufanyika February 6 mwaka huu.

Meneja wa uhusiano wa Multichoice Furaha Samalu alisema kwamba Lilian amefanikiwa kupita hatua ya kumi (10) bora baada ya kupita mchujo wa washiriki wengine 24 kutoka nchi mbali mbali.

Kabla ya kupatikana kwa washiriki kumi warembo hao walikuwa kambini nchini Kenya katika mji wa Mombasa katika kambi maalumu.

Lilian anatarajiwa kuondoka tarehe 26 kuelekea Afrika Kusini tayari kwa fainali hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Nigeria katika mji wa Lagos.

Zaidi ya hayo mbunifu wa kitanzania anayeishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini Anisa Mpungwe amepata nafasi ya kuwaandalia mavazi baadhi ya washiriki watakaoshiriki kwenye fainali hizo.

Lilian ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es salaam amewaahidi watanzania kufanya makubwa na kufwata nyao za dada yake Miriam Odemba kama ilivyokuwa mwaka 1999.






WAJUE MACELEBRITZ WA TANGA CITY!! (PART 2)

Aliyevaa T Shirt nyeupe anaitwa Eddy Eville, bosi wa Super Starz Entertainment, wa kati kati ni Tiny Daddy ni mtangazaji wa Breeze Fm Radio pamoja na Dj Bob Nass wa Breeze Fm Radio ya hapa jijini Tanga.

Ras Bazzle wa Mwambao Fm Radio akiwa na msanii Dulla Wa Michano kutokea Tanga City

Katika Pozz anaitwa Man Sasha mzee wa Magumashi, mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri jijini Tanga





Friday, January 22, 2010

ALBUM YA DIAMOND SOKONI SIKU YA VALENTINE (14/02/2010)

Msanii wa Bongo Flava anayetamba na kibao chake acha "Nenda Kamwambie" kinachofanya vizuri kwenye Radio na Tv muite Diamond, anatarajia kuachia albamu siku ya Valentine yaani tarehe 14/02/2010.

Albam hiyo yenye nyimbo kumi na mbili inaitwa KAMWAMBIE, wasanii walio pata shavu la kuwemo katika albam hiyo ni pamoja na Ngwair, Hemedy, Mabovu, Blue, Fatma na wasanii chipukizi. Mzigo umekamilika katika studio tofauti ikiwemo Sharobaro Rec, 41 Rec, Fish Crub Rec, pamoja na Sei Rec. Jukumo lote la kusambaza albam hiyo imeachiwa kampuni ya FM WASAMAZAJI

"KWA AJILI YAKO" ALBAMU YA HUSSEIN MACHOZI INAYOFANYA VIZURI MTAANI

Machozi amesema albamu yake ni mfano wa kuigwa kwa sababu nyimbo zake zinagusa kila rika na zina ujumbe mbalimbali muhimu kwa jamii. Pia alisema ujumbe wake unagusa maisha ya kila siku ya jamii.

(Akiwa na Prof Jay, na Kassim) Msanii huyo mwenye sura yenye mvuto alisema, ameamua kutoa albamu hiyo mapema, kufuatia maombi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki wake waliopo katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Alivitaja vibao vilivyomo kwenye albamu hiyo kuwa ni ‘Yes we can’ alichomshirikisha msanii Bonta, ‘Utaipenda’ alichomshirikisha Joe Makini, ‘Kabla ya jua kuzama’ alichomshirikisha Mac d, ‘Niacheni niseme’ na ‘Full shangwe remix’ alichomshirikisha AY. Vingine ni ‘Kwa ajili yako’, ‘Za mwizi 40’, ‘Dont cry’, ‘Karibu narudi’ alichomshirikisha Farida na ‘My wife’.

PIGA NAMBA HII KUPATA ALBAMU YA HUSSEIN MACHOZI 0713 131073






FADDY DADDY MKALI WA BONGO FLAVA KUTOKEA TANGA CITY!

Msanii kutoka mkoani Tanga Faddy Dady, akiwa katika Pozz punde baada ya kufanya Interview kwenye kipindi cha The Hot Beat kinachorushwa na Mwambao Fm Radio hapa jijini Tanga. Faddy ambaye amewahi kutamba na wimbo wa "Moyoni Naumia" ambao ulimtambulisha vizuri kunako game ya muziki wa Bongo Flava.

Hapa akiwa na Dj Roja Kiss wa Mwambao Fm. Faddy sasa anatamba na ngoma yake kali ya "Asali Shubiri" aliyoirekodi kwa producer Steve White chini ya studio Land Line Production.

(Akiwa na Dj Roja Kiss na Dj Bob Nass wa Breeze Fm Radio) Mchizi hivi sasa yupo chuo pale mlimani anapiga buku na ametanabaisha kuwa albamu yake ya "NIMEUPATA VIPI" ipo sokoni kwa hiyo unaweza kujipatia copy yako. Faddy amemalizia kuwa anatarajia kuachia singo yake ya tatu wiki ijayo ambayo ameifanya pale Akinato Record chini ya producer lil Gheto.







Wednesday, January 20, 2010

WAJUE MACELEBRITZ WA TANGA CITY!!

Aliyevaa Red Shirt anaitwa Ally Mohammed a.k.a Bra A, mtangazaji wa Mwambao Fm. Anayefuatia anaitwa Ras Bizo a.k.a Babaizoo, mtangazaji wa Mwambao Fm pia. Aliyevaa T shrt nyeupe anaitwa Edmund Aloyce a.k.a Dj Bad Fuvu (Kichwa Kibovu) dj wa Mwambao fm radio. Pamoja na wana wengine.

Wapo wengi usiowafahamu! Wanafanya nini na ishu gani wanatarajia kuzifanya katika future plan zao....achilia mbali wasanii wa muziki. Utawajua watangazaji wanaotamba, wacheza filamu na hata wale wenye majina hapa Town!

Anko Mo Blogspot itakukuletea Macelebritz wa Tanga City ili upate kuwajua na kusoma vijimambo vyao kupitia hapa. Kila kukicha Tanga imekuwa ikitoa macelebritz wanaotambulika Tanzania na dunia kwa ujumla.

Kaa Tayari!!!!







Tuesday, January 19, 2010

"SIWEZI KUMNYOOSHEA MTU KIDOLE WAKILISHA"- SHAA

Aniatwa Shaa kifupi cha jina alilolitumia kipindi yuko na kundi zima la Wakilisha lililokuwa linaundwa na vijana watatu Witness Mwaijaga, Langa Kileo na yeye Mwenyewe Sarah.

Akiongea wakati akijibu swali la nini kilichopelekea kuvunjika kwa kundi la Wakilisha Sarah alisema ya kuwa hawezi kumnyooshea mtu kidole kuwa alihusika moja kwa moja kuvunjika kwa kundi hilo kwani hata yeye alihusika.

“Siwezi kumnyooshea mtu kidole kwasababu hata mimi nilihusika katika kuvunjika kwa kundi,” alisema Sha ambaye alikuwa wa kwanza kujitoa katika kundi hilo kabla memba waliosalia nao kila mmoja kushika njia yake.

Muimbaji huyo amesema utoto ulikuwa umetawala wakati huo na hivyo akajikuta akisikiliza maneno ya uzushi kutoka kwa watu na kujikuta akichukua uamuzi wa kujitoa kundini.

Baada ya Sara, ambaye alikuwa akiimba viitikio vya nyimbo za Wakilisha kujitoa kundini, memba waliosalia Witness na Langa wakalipunguza jina lao na kujiita Wakili na wakarekodi wimbo ulioitwa ‘No Chorus’, ambao kama jina lake lilivyo haukuwa na kiitikio.

Sara hakuona sababu ya kuacha historia yote ya Wakilisha ifutike katika sanaa yake baada ya kujitoa kundini, hivyo baadaye akaamua kuchukua jina lililotemwa na wenzake kutoka kwenye jina la Wakili - SHA.


“Hata hivyo, sikugombana na yeyote miongoni mwa memba wa kundi,” alisema Sha.“Ndio maana katika nyimbo zangu ninazoandaa sasa, nawashirikisha wote wawili ili kufuta hisia zozote mbaya zinazoweza kuwepo kufuatia kuvunjika kwa Wakilisha.”

Sha amesema anaendelea vyema katika maandalizi ya albam yake ya kwanza tangu aanze muziki lakini hataki kuizungumzia sana kwasababu iko katika hatua za mwanzo.“unajua mimi napenda vitu vilivyo kamili, hivi sipendi kuzungumzia vitu ambavyo havijakamilika.” alimalizia Shaa







Monday, January 18, 2010

TANGA VILLAGES TO BENEFIT FROM MCC PROJECT!

Over 70 villages in Tanga region would get electricity through a Millennium Challenge Corporation (MCC) sponsored project to be implemented by the Tanzania Electricity Supply Company (Tanesco).
The Tanesco regional engineer, Mr Martin Ngelege, said here that the project would improve power supply in some villages as one of several projects to be financed by MCC. Mr Ngelege said that the project would be implemented in phases and preparations for implementation of the first phase have been completed.

The preparation includes survey and evaluation aimed at preparing payment of compensation in the 77 villages that would be involved in the project. A total of 27 villages would be covered by the project in Lushoto district.
Tanga City would have 19 areas covered while 14 villages would benefit in Muheza district. Handeni and Korogwe would have seven villages each and from Pangani three villages would be connected.

Other MCC sponsored projects include construction of new transformers stations at Saruji and Sahare in the Tanga City and Kasiga Mombo in Korogwe district. The project would also involve rehabilitation of the main power distribution station at Songa.
Tanga is one of five regions where the MCC funded projects would be implemented. The projects aim at improving power supply services in Tanzania.

Some $206 million (about Sh273.9 billion) will be used to sponsor several projects aimed at improving electricity supply in several parts of the country. The projects are part of a three-year programme to rehabilitate and expand power supply and distribution systems using local and donor funds.

They include a project aimed at improving power transmission to Zanzibar using submarine cable, constructing 8MW power supply project at Malagarasi River and improving electricity supply to Kigoma Region. The funds would also be used for rehabilitating worn out power distribution systems in six Tanzania Mainland regions of Mwanza, Tanga, Morogoro, Iringa, Dodoma and Mbeya.




"TUNAJITANUA ZAIDI"- P FUNK

Studio kubwa ya kurekodi muziki nchini Bongo Record iliyopo chini ya Producer maarufu nchini P Funk a.k.a Majani hatimaye imeamua kufanya kitu tofauti kabisa na ndio itakuwa ya kwanza kabisa nchini kuanza kurekodi miziki kwa ajili ya kutengenezea Filamu.

Majani amesema kuwa wameamua kwenda mbele zaidi sio tu kwa kutaka hela anataka awaonyeshe watanzania ni jinsi gani wao kama Bongo Record wanaweza kufanya kitu kingine zaidi ya kurekodi tu.


“Hii ni kitu mpya kabisa nadhani Bongo Record ndio tutakuwa wa kwanza kuanzisha kitu kama hiki, tutakuwa tunafanya kwa Filamu pia na Documentary” alisema P Funk ambaye kwasasa yuko kwenye mojawapo ya kazi hiyo.

Zaidi ya hayo P Funk alisema muziki wa kibongo pia umeingiliwa na umevamiwa na ma producer wengi ni uchwara na ni mojawapo ya sababu ya yeye kufanya kitu tofauti kidogo.


Friday, January 15, 2010

"HAKUNA KUOGOPA POLISI" NGOMA MPYA YA MADEE

Msanii wa kundi la Tip Top Connection Madee ambaye ni rais wa Manzee jina la paspot, Ahmad Ally amesema kuwa yupo tayari kuachia ngoma yake mpya aliyoupa jina la ‘Hakuna kuogopa polisi’.

Madee alisema kibao hicho kinachozungumzia masuala mbalimbali ya kiusalama amekirekodi katika studio za Dhahabu zinazomilikiwa na msanii Dully Sykes.

Alisema kibao hicho ambacho kinapatikana kwenye albamu yake aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana ‘Pesa’ atakisambaza rasmi kwenye vituo mbalimbali vya redio wiki ijayo.

“Ni kibao kizuri na chenye ujumbe kwa jamii, kama kawaida Madee huwa sibahatishi kazi zangu...mashabiki wangu wasubiri kupata uhondo ndani ya kibao hicho,” alisema.

Thursday, January 14, 2010

MAANDAILIZI YA KAMPENI MAALUM YA KUTOKOMEZA MALARIA YAZIDI KUIVA!

Maandalizi ya Kampeni maalumu ya kutokomeza Malaria yaanza kwa kishindo Ikulu.

Wadau Ally Rehmtullah na Prof Jay wakiwa tayari katika kampeni maalumu ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria.
Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku ya Jana ofisini kwake Ikulu kwa ajili maandalizi ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria. Kampeni hiyo inayojulikana kama ZINDUKA inatarajiwa kuzinduliwa Februari 13 mwaka huu wa 2010.