BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, February 1, 2010

BWAGAMOYO INTERNATIONAL KUANZA KAZI RASMI

BENDI ya Muziki wa dansi inayoongozwa na mwimbaji mahiri nchini,Muumini Mwinjuma (Kocha wa Dunia) Bwagamoyo International inaingia studioni wiki hii kurekodi nyimbo zake tatu mpya.

Katika nyimbo hizo.Bwagamoyo inataraji kurekodi pia wimbo unaotazamiwa kuwatoa machozi wasikilizaji na watazamaji wa televisheni, ujulikanao kwa jina la Nafsi haina urithi ambao unawataja watu mbalimbali waliokwishaaga dunia akiwamo Rashid Kawawa .

Bwagamoyo ambayo ipo kambini Chumbageni Tanga ikiwa na vyombo vipya vya kisasa vilivyoletwa nchini hivi karibuni kutoka Ujerumani iatarekodi nyimbo hizo katika studio ya Tanzania Youth Aliance iliyopo Kinondoni Jijini Dar es saalm.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika kambi ya Jijini Tanga, Mkurugenzi wa Bwagamoyo,Muumini, alisema bendi hiyo imeasukwa upya kwa lengo la kuleta ushindani katika soko la muziki huo nchini na nje ya nchi .

Alizitaja nyimbo zitakazorekodiwa kuwa ni Mwanamtili Malunde na Nafsi haina urithi zilizotungwa nay eye Muunimi akishirikiana na Dr Rama,pamoja na Undugu wa mashaka ukiwa ni utunzi wa Venance Joseph ambaye pia ni Rais wa bendi hiyo inayotumia mtindo wa gusa unase.

"Wimbo wa Nafsi haina urithi unaelezea jinsi ndugu wanavyositikika wanapofiwa na mtu wanayempenda lakini ni vigumu kumfuata kwa kuwa kaburi lake ni nyumba ndogo ya mmoja tu,na tumewakumbuka wenzetu kadhaa waliotutoka"alisema Muumini

“Bwagamoyo International imesukwa upya inao wanamuziki mahiri waliojiunga kutoka bendi nyingine na pia imepata wanenguaji tishio”alisema Muumini na kusita kuwataja kwa maelezo kuwa baadhi yao hawajakamilisha mipango ya kutoka kwenye bendi zao za awali.

Wanamuziki watakaoingia studio na bendi hiyi ni pamoja na waimbaji,Venance Joseph,Mrisho Rajab,Asha Rajabu,Asha Hassan na Mwamvita Katundu wakiwa na mfokaji Maneno Mohamed (Buster).

Gitaa la solo linakung’utwa na Hemed Yassin,Yahaya Makango (Rhyizi)m,na George Gama (Bass) na Keybody Kally huku Drums na tumba zikipigwa na Patrick Clayery na Hamza Salehe. .

Wanenguaji waliopo katika kikosi hicho ambao watashiriki kurekodi kwenye televisheni ni ni Queen Happy,Sauda Said,Tausi Yahaya na Ratifa Said wakiwa chini ya walimu Chino Loketo na Small Kabwe.

Bendi hiyo imejizolea mashabiki baada ya kufanya ziara katika mikoa ya Kanda ya ziwa ambako ambako miongoni mwa nyimbo zilizopigwa ni Tunakukumbuka mama,Manyanyaso yatima,undugu wa mashaka,Nani kama mama,Natafuta mume na Quity baby.

Alisema baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi,wanamuziki wa bendi hiyo watarejea Tanga kuendelea na kambi yao tayari kuisuka zaidi.


HABARI NA OSCAR ASSENGA




No comments:

Post a Comment