BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, April 15, 2010

BREAKING NEWS!!!!!!.......DULY NAE AJITOA TUZO ZA KILI!!

Msanii Dully sykes aka Mr Misifa nae ametamka rasmi kujitoa tuzo za Kili.

"Nimesema na nilishasema sitaki kuwekwa katika category yoyote ile ya KIli Music Award, sioni faida ya tuzo hizo, sijawahi kupata tuzo tangu nianze mziki, single 36 mpaka sasa kama Salome,Hunifahamu na nyinginezo kibao zilizobamba lakini cha ajabu hakuna hata moja nimepata tuzo.....ni bora nitoe single tu na wala hata album sitaki."

Hayo yalikuwa maneno ya Mr Misifa alipokuwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio. Dully alikuwa katika Category ya wimbo bora wa Ragga, ambapo alikuwa akichuana na wasanii wengine kama Bwana Misosi (Mungu yuko Bize), Drezzy Chief (Wasanii) na Benjamin wa Mambo Jambo (Fly)

Dully amekuwa msanii wa pili kujitoa baada ya T.i.d kujitoa wiki mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment