BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, April 28, 2010

'SIWAIMBII MADEMU ZANGU WA ZAMANI'- KASSIM



Siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari iliyomhusu msanii mmoja kutoka katika kundi la Tip Top Connection Hemed Mganga a.k.a Cassim kuwa katika tungo zake amekuwa akiimbia wanawake zake wa zamani, ameibuka na kudai kwamba taarifa hizo si za kweli.

Kwa masikitiko makubwa msanii huyo amesema kuwa yeye hana marafiki wa karibu kiasi kwamba wanaweza wakajua A-Z kumhusu.

"Sina marafiki wa namna hiyo licha ya hivyo sina na sijawahi kuwa na msichana ambaye ana jina linalofanana na majina ya wasichana ambao huwa ninawaimba kwenye tungo zangu" alisema.

"Ujue siku zote muziki ni kama ufahamu wa mtu, na kile mtu anachokipenda, hivyo unapokuwa unaandaa tungo yanakuja majina mbalimbali kichwani na si kila msanii fulani anachoimba basi ni maisha yake halisi, hapana pale tunaelimisha na kuburudisha jamii na si vinginevyo" alisema.

Alisema kuwa akiwa kama msanii anatambua nini anafanya na mchango gani unahitajika katika jamii hivyo hawezi kufanya yaziyofaa.

Cassim amekana tuhumu zinazomkabili kuwa amekuwa akiwaimba wasichana wake ambao amekuwa na mahusiano nao hapo awali, majina yaliyotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Awena, Cindy, Amore.

No comments:

Post a Comment